• Utafiti huo ulionesha kuwa gharama ya intaneti nchini Uganda ni ya bei nafuu ikilinganishwa na mataifa mengine.
Utafiti wa awali ulionesha kuwa Kenya inaongoza kwa wamiliki wa simu lakini kwa kufikia intaneti, Uganda inawapiku.
Mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya CA imetoa takwimu mpya za utafiti wa matumizi ya mitandao ya kijamii katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Katika utafiti huo, Kenya na Tanzania kuenea kwa mawasiliano ya mtandao wa simu za mkononi unafuata nyuma ya Uganda, ambayo ina kiwango cha juu zaidi cha kupenyeza kwa mtandao wa simu za mkononi.
Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) zinaonyesha Uganda ilikuwa na upenyaji wa mtandao wa simu wa asilimia 46.88 kufikia Juni 2021 na kushinda asilimia 46.76 ya Kenya.
Sudan Kusini ilikuwa ya mwisho kati ya nchi hizo sita, Burundi ilikuwa ya pili kwa kiwango cha chini cha upenyaji wa mtandao wa simu wa asilimia 10.96 huku Rwanda na Tanzania zikiwa na asilimia 42.84 na asilimia 14.31 mtawalia.
"Uganda iko mbele ya mataifa sita katika upenyezaji wa mtandao wa simu wakati Sudan Kusini ndiyo nchi ya chini zaidi kwa mawasiliano ya simu za rununu, Intaneti, na mtandao wa intaneti," ilisema CA katika taarifa.
Haya yanajiri licha ya Kenya kuzishinda nchi nyingine za EAC katika kupenya kwa simu za rununu.
Simu za rununu zilifikia asilimia 114 katika kipindi hicho ikilinganishwa na asilimia 61 tu nchini Uganda, asilimia 86 nchini Tanzania na asilimia 82 nchini Rwanda.
Lakini kiwango cha chini cha upenyezaji wa mtandao wa intaneti wa simu wa Kenya ikilinganishwa na Uganda licha ya kupenya kwa juu zaidi kwa simu za mkononi kunaweza kuashiria kwamba gharama ya kitengo cha Kenya cha mtandao wa simu ni kubwa kuliko Uganda, na hivyo kuzorotesha matumizi ya huduma za mtandao wa simu za mkononi.