logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ajuza wa miaka 95 amkumbatia kwa furaha kijana wake aliyemaliza kifungo miaka 20 jela (Picha)

Kang'ethe alikuwa akihudumia kifungo katika gereza kuu la Nakuru.

image
na Radio Jambo

Habari27 January 2023 - 13:10

Muhtasari


• Kang'ethe alihukumiwa miaka 20 jela baada ya kupatikana na kosa la ubakaji.

Joseph Kang'ethe akikumbatiana na mamake mkongwe baada ya kurudi nyumbani akitoka jela alikokaa miaka 20

Ilikuwa ni isiyo ya kawaida, siku ya furaha katika eneo bunge la Kuresoi Kaskazini, kijiji cha Mukinduri katika familia ya ajuza mmoja wa miaka 95 baada ya kijana wake kurejea kutoka jela alipohudumia kifungo cha miaka 20.

Joseph Kang’ethe mwenye umri wa miaka 69 sasa alihukumiwa miaka 20 iliyopita akiwa na miaka 49 katika gereza kuu la Nakuru.

Kang’ethe alipatikana na makossa ya ubakaji ambapo kifungo hicho kilimhusu.

Katika picha ambazo mpiga picha wetu alichukua, Kang’ethe na mama yake mkongwe walionekana wakikumbatiana kwa mapenzi ya mtoto kwa mama, huku ajuza huyo akipiga bismillah kwa kumuona tena mtoto wake ambaye walikuwa wametenganishwa naye kwa miongo miwili iliyopita.

Baada ya kuwasili nyumbani, Kang’ethe alipewa karibu kama shujaa kwani watu wengi walifurika nyumbani kwake kumuona kama kweli yuko mzima, kwani wengi walikuwa wanafikiri kama kioja kumuona mzee aliyehudumia kifungo cha miaka mingi na kurejea nyumani akiwa salama na aliyebadilika kimaadili.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved