Alinikana mbele ya 'mubaba' wake-Mwanamume asimulia alivyopigwa chenga na mpenziwe

Kulingana naye aliona mpenzi wa maisha,ila mwanamke huyo alikuwa anataka pesa tu na mali yake.

Muhtasari
  • Nikiwa kwenyez iara yangu nilipatana na mwanamume ambaye alipatwa na msongo wa mawazo baada ya kuachwa na mpenzi wake
stress (1)
stress (1)

Katika ulimwengu wa sasa asilimia kubwa ya wanawake na wanaume waliopitia kwenye upande wa mapenzi na kutofauli kwa hakika watakupa hadithi jinsi walivyo umizwa moyo.

Kuna wale huendelea na maisha yao na kuamua kwamba liwe liwalo watapenda tena, lakini baadhi yao ukata tamaa na kuamua kuendelea na kazi zao.

Nikiwa kwenyez iara yangu nilipatana na mwanamume ambaye alipatwa na msongo wa mawazo baada ya kuachwa na mpenzi wake.

Kulingana naye aliona mpenzi wa maisha,ila mwanamke huyo alikuwa anataka pesa tu na mali yake.

Huku akisimulia yaliyompata alisema;

"Nikiwaita baadhi ya wanawake 'daughters of Jezebel' huwa nahisi vyema kwani nilitendwa na mwanamke ambaye nilikuwa napenda sana.nilimchumbia mwanamke kwa miaka 4 kumbe alikuwa anataka tu mali na pesa yangu 

Nilimpata na mwanamume mwingine kisha nilipomuuliza alinikana mbele yake na kudai kuwa mimi ni binamu yake,kisha alimuamuru 'mubaba' wake anifukuze kama mbwa mahali walipokuwa wakijivinjari,si kuwahi fikiria tutakuja kuachana ata siku moja

Nilipatwa na msongo wa mawazo kwa mwaka 1, kabla ya kuenda kumuona mshauri,niliapa kutojihusish na ujinga kama huo ambao watu wanasema ni mapenzi,nilifikiri mambo mengine ni ya filamu tu lakini yalinipata na kwa kweli 'experience is the best teacher'."

Akiwashauri wenzi na wanandoa alisema;

"Kama unampenda mwenzi wako mpende lakini usijaribu kuumiza hisia za mwenzio kwani huyo ni binadamu pia,kwa wale wako kwenye ndoa jueni kwamba ndoa inapaswa kupewa heshima na wala sio kusumbuana kila kuchao na baadhi yenu kutafuta mipango ya kando."

Siku ya Ijumaa mahakama ya juu ilisema kwamba katika kesi ya talaka, kila mhusika anapaswa kuacha ndoa na mali aliyoipata wakati wa muungano ingawa mwenzi anaweza kupata zaidi kulingana na mchango wake katika ndoa na upatikanaji wa mali ya ndoa.

Mahakama ya majaji watano ikiongozwa na naibu jaji mkuu Philomena Mwilu pia ilishikilia kuwa kila mwenzi katika ndoa lazima athibitishe mchango wake katika utajiri wa familia ili kuwezesha mahakama kuamua asilimia inayopatikana kwake katika ugawaji wa mali ya ndoa.

Mahakama ilisema kuwa mtihani wa kuamua kiwango cha mchango wa mhusika ni mojawapo ya msingi wa kesi.

Haya basi kwa wanawake ambao wanawapenda wanaume kwa ajili ya mali wamepata pigo lao.