logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Mungu ametwanga maadui wangu!" - Sonko baada ya Murathe na Kioni kutemwa Jubilee

Sonko alitimuliwa kama gavana miaka michache iliyopita na huenda tatizo lilianzia hapo.

image
na Davis Ojiambo

Habari11 February 2023 - 12:06

Muhtasari


  • • Kioni na Murathe walisimamishwa na nafasi zao kuchukuliwa na Kega na Keynan mtawalia.
Sonko mawinguni Kioni na Murathe walisimamishwa kazi

Aliyekuwa gavana wa Nairobi, mfanyibiashara Mike Sonko ameonesha furaha yake baada ya wanachama wa Jubilee kupiga kura kuwaondoa madarakati naibu mwenyekiti David Murathe na katibu mkuu Jeremiah Kioni.

Ijumaa alasiri, chama hicho kinachoongozwa na rais mstaafu Uhuru Kenyatta kiliandaa mkutano wa wanachama na kutoa taarifa kwamba wawili hao wamevuliwa madaraka.

Baada ya kuwavua madaraka wawili hao ambao wana ukaribu na kiongozi wa Azimio Raila Odinga, Jubilee walitangaza kuwa wako katika hatua za mwisho kuondoka katika muungano wa Jubilee.

Sonko kupitia kurasa zake mitandaoni alionesha furaha akisema kwamba Mungu ameamua kuwatwanga vikali maadui wake mwaka huu.

“Kwani Raundi hii Mungu ameamua kumenyana na Maadui wangu. JUBILEE NEC yawasimamisha kazi makamu mwenyekiti David Murathe na katibu mkuu Jeremiah Kioni; inatangaza kuwa iko njiani kutoka kwa muungano wa Azimio,” Sonko alinukuu maneno ya jarida moja la humu nchini.

Japo Sonko hakusema ni nini wawili hao walimfanyia mpaka kufuzu kuwa maadui wake, alisisitiza kuwa waliwahi kuwa na mkwaruzano mkali na naibu mwenyekiti David Murathe akisema kwamba alikuwa kama donda ndugu kwake.

Baadhi walihisi wawili hao walikuwa katika mstari wa mbele kwa matatizo yaliyomkumba Sonko kupelekea kutimuliwa kwake ofisini kama gavana wa Nairobi.

Baada ya kuwatimua wawili hao, Mbunge wa EALA Kanini Kega alichukua nafasi ya Kioni kama katibu mkuu kikaimu huku Adan Keynan akichukua nafasi ya Murathe kama naibu mwenyekiti kikaimu pia.

Sasac inasubiriwa kuonwa ni hatua gani Kioni na Murathe watachukua ikizingatiwa kuwa huenda hawakuwa katika mkutano huo na kauli yake muda mchache baadae kuwa chama hicho kitasalia ndani ya Azimio wala hakiondoki.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved