logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwalimu achomwa kisu na mwanafunzi hadi kufa

"Leo ni wakati wa simanzi na mshikamano," alisema alipotembelea shule hiyo.

image
na Radio Jambo

Makala23 February 2023 - 08:40

Muhtasari


  • Mwendesha mashtaka ataleza katika mkutano na wanahabari alhamisi kuwa atatoa maelezo zaidi kuhusu uchunguzi huo
Crime scene

Mwanafunzi wa shule ya sekondari amemchoma kisu mwalimu hadi kufa katika shule moja katika mji wa Saint-Jean-de-Luz nchini Ufaransa.

Msemaji wa serikali ya Ufaransa Olivier Véran alithibitisha shambulio hilo la Jumatano na kusema kuwa mshukiwa alikuwa na umri wa miaka 16.

Polisi walifika shule ya Saint-Thomas d'Aquin pamoja na mwendesha mashtaka wa eneo hilo, ambapo mwanafunzi huyo alikamatwa.

Gazeti la Kifaransa la Sud Ouest lilisema mshambuliaji huyo aliingia darasani wakati mwalimu alipokuwa akifundisha Kihispania na kumshambulia.

Mwalimu huyo alikuwa na umri wa miaka 50 na alikufa kwa mshtuko wa moyo baada ya huduma ya dharura kufika shuleni, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Kituo cha Televisheni cha Ufaransa BFM kilisema mshambuliaji alifunga mlango wa darasa na kumchoma kisu mwalimu kifuani.

Mwendesha mashtaka wa eneo hilo Jerome Bourrier alisema kuwa uchunguzi umefunguliwa na polisi wa eneo hilo kwa mauaji na mshukiwa yuko kizuizini.

Mwendesha mashtaka ataleza katika mkutano na wanahabari alhamisi kuwa atatoa maelezo zaidi kuhusu uchunguzi huo.

Waziri wa Elimu wa Ufaransa Pap Ndiaye amelitaja shambulio hilo kuwa "janga lenye uzito wa kupindukia" na kutuma salamu zake rambirambi.

"Leo ni wakati wa simanzi na mshikamano," alisema alipotembelea shule hiyo. "Taifa zima lipo hapa kuelezea huzuni na hisia zake."

 

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved