logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bilioni 34 za ruzuku ya mafuka zilipotelea mifukoni mwa watu ndani ya miezi 15, ripoti

Ukaguzi huo unamweka aliyekuwa waziri wa fedha Ukur Yatani kwenye kikaango.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri06 March 2023 - 06:24

Muhtasari


• Kulingana na wadadisi wa hesabu, fedha hizo zilikuwa na uwezo wa kujenga madarasa 17000.

Pesa za Kenya

Uchunguzi umebaini kwamba takribani bilioni 34 ambazo serikali ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta ilitenga kama ruzuku kwa mafuta zilipotelea katika mifuko ya watu binafsi ndani ya kipindi cha miezi 15.

Ruzuku hiyo ambayo serikali ya Kenyatta ilitenga ili kuwalinda Wakenya kutokana na bei za juu za mafuta kutokana na mfumuko wa kiuchumi zinasemekana kupotea kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti mwaka jana.

Kulingana na wachambuzi wa fedha katika Ofisi ya Bunge ya Bajeti, pesa hizo zina uwezo wa kujenga visima vya maji kot nchini visivyopungua idadi ya 3400 au kujenga madarasa yapatayo 17000.

Kulingana na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Nancy Githungu, Upotevu huu wa fedha ni pamoja na Shilingi milioni 554.72 zilizolipwa zaidi kwa kampuni 11 za uuzaji wa mafuta (OMCs).

Ukaguzi huo maalum ulihusisha kipindi cha Aprili 1, 2021 hadi Juni 30, 2022 na umeashiria njia mbalimbali ambazo huenda fedha za umma ziliibwa ama kwa tume au kutotekelezwa na maafisa wa serikali.

Ukaguzi huo maalum unamweka waziri wa Hazina ya Kitaifa wakati huo kweney kikaango juu ya Shilingi bilioni 22.68 kutoka PDLF. Sheria ya PDLF ya 1991 inataka pesa za mfuko zitumike katika uundaji wa vifaa vya usambazaji au majaribio ya bidhaa za mafuta.

Sheria iliyoanza kutumika Julai 15, 2020, inaeleza zaidi kwamba fedha hizo pia zitatumika kwa utulivu wa bei ya pampu ya petroli ya ndani katika matukio ya ongezeko la gharama za kutua juu ya kizingiti kilichowekwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (Epra)


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved