logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kama hana gari subaru za DCI zimpe lift-Cherargei kwa Matiang'i

"Matiangi anaweza kukimbia lakini hawezi kujificha lazima aheshimu wito wa DCI

image
na Radio Jambo

Burudani06 March 2023 - 14:35

Muhtasari


  • Wakili wa aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i Danstan Omari aliwasilisha hati ya wito

Seneta wa Nandi Kiprotich Cherargei amejibu kupitia ukurasa wake rasmi wa twitter saa chache baada ya DCI kumwita aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi.

Wakili wa aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i Danstan Omari aliwasilisha hati ya wito iliyomtaka mteja wake kufika JUmanne katika makao makuu ya DCI saa 9:30 asubuhi.

"Matiangi anaweza kukimbia lakini hawezi kujificha lazima aheshimu wito wa DCI kama alivyokuwa akisisitiza alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Kama hana gari subaru za DCI zimpe lift mpaka DCI headquarters in company of Tinga kesho mangware.Nilisema alambe glucose safari bado ni mbaaaaali sana". Alisema Mhe. Kiprotich Cherargei.

DCI inayoongozwa na mpelelezi Micheal K. Sang awali ilisema kwamba wanachunguza madai ya taarifa za uongo za umma kuhusu madai ya kuvamiwa na polisi katika Nyumba yake ya Karen usiku wa kuamkia Februari 8, 2023.

Baadhi ya Wakenya wanadai kuwa rais William Ruto na washirika wake wanamlenga aliyekuwa katibu mkuu wa baraza la mawaziri kuhusu jukumu alilotekeleza wakati wa utawala uliopita.

Mpelelezi anasema Kushindwa Kuzingatia ombi kunajumuisha kosa linalowajibika kufunguliwa mashtaka.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved