Watu 4 hufariki kila baada ya saa moja kutokana na makali ya HIV/AIDS, ripoti

Wizara pia ilisisitza kwamba maombi kwa wachungaji na wahubiri hayawezi kutibu HIV, na kuwataka waathiriwa kuendelea kutumia ARV.

Muhtasari

• Taarifa ya baraza hilo pia ilibainisha kuwa vifo 760,314 vimeepukika na Tiba ya Kuzuia Ukimwi (ART).

Mchoro wa ukimwi
Mchoro wa ukimwi
Image: The Star

Baraza la kitaifa la kudhibiti maambukizi ya Ukimwi limetoa takwimu za kushangaza kwamba angalau watu 4 hufariki kila baada ya saa moja kutokana na makali ya virusi vya Ukimwi.

Kulingana na ripoti ya siku ya Ukimwi Duniani ya 2022, Virusi vya ukimwi vilichangia asilimia 29 ya vifo vyote nchini. Kati ya kila watu wanne walioambukizwa KIV kwa saa mmoja alikuwa mtoto.

Taarifa ya baraza hilo pia ilibainisha kuwa vifo 760,314 vimeepukika na Tiba ya Kuzuia Ukimwi (ART).

Wakati huo huo, maambukizi ya watoto 164,072 yalizuiliwa kutokana na mpango wa Kuzuia Maambukizi kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto.

Kaunti zilizo na maambukizi ya juu zaidi zilikuwa kama ifuatavyo: Kaunti ya Homa Bay ndiyo iliyokuwa na maambukizi ya KIV kwa asilimia 16.2, Kisumu (15.5%), Siaya (14.1%), Migori (10.4%), Busia (5.4%), Mombasa (5.4%). ), Kisii (4.7%), Samburu na Vihiga (4.6%), Nairobi (4.3%) na Uasin Gishu (4.0%).

Ripoti hiyo pia ilisema kuwa kuna mapuuza kwa baadhi ya watu kukosa kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo huku ikisisitiza kwamba maombi kamwe hayawezi kutibu virusi vya ukimwi.

Mwezi jana, kulikuwa na mjadala mkali mitandaoni mchungaji mmoja maarufu nchini akidai kwamba aliwaponya mamia ya watu ambao walitafuta maombi katika mkusanyiko wake mkubwa na ambao walikuwa waathirika wa virusi vya ukimwi.

Wizara ya afya pia iliwataka walokole kutokosa kuhudhuria maombi lakini pia wasikose kutumia dawa za ARV kama wana virusi vya UKIMWI.

Mchoro wa ukimwi
Mchoro wa ukimwi
Image: The Star