Maneno yaliyotumiwa na adui dhidi yetu hayapaswi kuvumiliwa-Muhoozi

Jenerali Muhoozi alidai kuwa ingawa Waafrika ni jamii kubwa zaidi duniani, kuna watu ambao walikuwa hawathamini hilo.

Muhtasari
  • Aliendelea na kudai kuwa baadhi ya watu walikuwa wakitumia lugha ya matusi kama "Nigga" kumaanisha "Watu Weusi" ambayo haifai kuvumiliwa hata kidogo.
KWA HISANI
KWA HISANI
Image: Muhoozi Kainerugaba

Mtoto wa Rais Yoweri Museveni ambaye ni Jenerali Muhoozi Kainerugaba amewasifu watu weusi akidai kuwa Waafrika ni watu wakuu.

Akitumia akaunti yake rasmi ya Twitter, Jenerali Muhoozi alidai kuwa ingawa Waafrika ni jamii kubwa zaidi duniani, kuna watu ambao walikuwa hawathamini hilo.

Aliendelea na kudai kuwa baadhi ya watu walikuwa wakitumia lugha ya matusi kama "Nigga" kumaanisha "Watu Weusi" ambayo haifai kuvumiliwa hata kidogo.

"Watu weusi wote ni wamaana! Sisi sote ni wazao wa watu wa kwanza! Kwa kweli, Waafrika ni jamii kubwa zaidi duniani! Maneno ambayo Adui aliyatumia dhidi yetu kama 'Nigga' HAYAPASI kuvumiliwa na sisi wenyewe! Lugha kama hiyo ni 'Marufuku'. ' kama tunavyosema kwa Kiswahili! Ni 'Haramu'." Jenerali Muhoozi Kainerugaba aliandika.

Muhoozi amekuwa kwenye vichwa vya habari kwa ajili ya maneno yake tatanishi kuhusu Afrika.

Jenerali huyo aligonga vichwa vya habari sana baada ya matamshi na madai yake ya kuteka nyara mji wa Nairobi.