logo

NOW ON AIR

Listen in Live

NASA yagundua jiwe linaloweza kuigonga dunia mwaka 2046

Uwezekano wa jiwe 2023 DW kugonga dunia unakadiriwa kuwa juu kuliko 1 kati ya 560.

image
na Radio Jambo

Makala12 March 2023 - 04:41

Muhtasari


•Kuna hatari ya jiwe jipya la asteroid 2023 DW lilogunduliwa na NASA kugongana na ulimwengu siku ya wapendanao mwakani 2046.

•Ikiwa jiwe hili litagongana na Dunia katika miaka 23 ijayo, athari yake itasababisha uharibifu mkubwa ikiwa litatua karibu na jiji kubwa au jamii

Katika siku ya wapendanao ya mwaka 2046, watu kote ulimwenguni wanaweza kulazimika kukusanyika ili kuona ikiwa, binadamu ataendelea kuishi? Kwa sababu kuna hatari fulani kwa jiwe jipya la asteroid 2023 DW lilogunduliwa na NASA kugongana na ulimwengu wetu siku hiyo

Hata hivyo, hatari ni ndogo kama 1 kati ya 625, kulingana na hesabu za Shirika la Anga la Ulaya (ESA). Uwezekano wa jiwe 2023 DW kugonga dunia unakadiriwa kuwa juu kuliko 1 kati ya 560.

Jiwe hilo kwa sasa ndiyo kitu pekee cha anga kilichoainishwa kama hatari ya Kiwango cha 1 kwenye Mizani ya Hatari ya Torino, ambayo ina mizani 10. Uchunguzi mwingine wa angani uliogunduliwa na NASA umeainishwa kama hatari kwa Dunia katika Kiwango cha 0, kumaanisha kuwa hauna nafasi ya kugonga dunia.

Maafisa wa NASA walisema hatari ya Asteroid 2023 DW ya Ngazi ya 1 inamaanisha kuwa haiwezekani kugongana na duniani. Lakini hatari hii ya chini sana inaweza kuongezeka. Wanaastronomia wanapopata fursa ya kufuatilia, kukusanya data na kurekebisha hesabu zaidi katika miaka kadhaa ijayo.

Hivi karibuni NASA iligundua asteroid 2023 DW mnamo Februari 27. Ilibainika kuwa ilikuwa na upana wa takriban mita 50, au ukubwa sawa na bwawa la kuogelea la Olimpiki. Kulizunguka jua kwa kasi ya kilomita 25 kwa sekunde, linachukua siku 271 kukamilisha obiti moja na kwa sasa liko karibu kilomita milioni 18 kutoka duniani.

Ikiwa jiwe hili litagongana na Dunia katika miaka 23 ijayo, athari yake itasababisha uharibifu mkubwa ikiwa litatua karibu na jiji kubwa au jamii. Kwa mfano, mlipuko wa meteorite wa 2013 juu ya jiji la Urusi la Chelyabinsk uliharibu majengo mengi na kujeruhi watu 1,500.

Hesabu za hivi punde zinaonesha kuwa jiwe hili litakuja karibu na Dunia kwa jumla ya mara 10 kati ya 2046 na 2054, na karibu zaidi ya dunia mnamo Februari 14, 2046 kwa umbali wa kilomita milioni 1.8.

Wiki iliyopita, NASA ilithibitisha mafanikio ya misheni ya DART, ambayo inaweza kutumia roketi kuzuia mawe na kugeuza njia zao. Hadi litakapokuwa nje ya mstari ambayo inahatarisha kugongana na ulimwengu. Lakini pia alikiri kwamba mbinu hiyo ilichukua miaka ya maandalizi. Kwa hiyo inaweza kuondoa vitu vya hatari anga za mbali.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved