Polisi 18 wa kike kitengo cha magereza wafutwa kazi kwa kupendana na wafungwa wa kiume

Ufichuzi ulionesha kwamba maafisa hao 18 wa kike walikuwa na mfululizo wa kushiriki mapenzi na wafungwa wa kiume kwa miaka 6 iliyopita.

Muhtasari

• Ufichuzi huo ulifanyika katika gereza la HMP Berwyn, moja ya magereza makubwa Zaidi yenye wafungwa wengi katika taifa hilo la Ukoloni.

• Afisa mkuu wa magereza alisema hilo lilitokea kwa sababu ya kuwapa watu wasiofaa kazi.

• Alibaini kwamba wengi wa maafisa hao waliajiriwa baada ya kufanyiwa usaili kupitia mtandao wa Zoom.

Mfungwa akiwa jela
Mfungwa akiwa jela
Image: Mfungwa Jela

Maafisa wa magereza wa kike wapatano 18 wamefutwa kazi kufuatia ufichuzi wa tuhuma kwamba walikuwa wanajihusisha kwenye vitendo vya mapenzi na wafungwa katika gereza moja nchini Uingereza.

Kulingana na jarida la Dail Mail, skendo hiyo iligundulika na kubaini kwamba maafisa hao wa magereza wamekuwa wakijihusisha katika vitendo vya mapenzi na wafungwa kwa Zaidi ya miaka 6 iliyopita.

Ufichuzi huo ulifanyika katika gereza la HMP Berwyn, moja ya magereza makubwa Zaidi yenye wafungwa wengi katika taifa hilo la Ukoloni.

Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Magereza, Mark Fairhurst, alilaumu uhusiano huo kwa kuajiri "aina mbaya ya wanawake."

Aliiambia Mirror, "Wafanyikazi wanaoajiriwa hawana mahojiano ya ana kwa ana... yote yanafanywa kwenye mtandao wa Zoom. Watu wengi wanaopata kazi hizi hawana uzoefu wa kutosha wa maisha na wana uwezekano wa kuwekewa masharti na wafungwa."

Miongoni mwa walinzi walio na hatia ya kuanzisha uhusiano na wafungwa katika gereza kuu la pauni milioni 250, ambalo lina wahalifu wa kiume wa Kitengo C, walikuwa Jennifer Gavan, 27; Ayshea Gunn, 27; na Emily Watson, 26, jarida hilo liliripoti.

Jennifer Gavan alifungwa jela miezi minane mwezi Disemba kufuatia mahusiano yake na mfungwa Alex Coxon, 25.

Upekuzi katika chumba cha kulala cha Gunn ulifichua mipigo ya wawili hao wakibusiana na kukumbatiana pia na picha za simu za mkononi zilizopigwa kwenye seli yake. Baadaye alifungwa mwaka mmoja katika Korti ya Mold Crown mnamo 2019.

 

Uhusiano huo ulikuja mwaka mmoja tu baada ya afisa mwenzake Ayshea Gunn, 27, kuchumbiana na mfungwa 'hatari' Khuram Razaq, 29.