Ajuza asimulia mjukuu wake kumfunga kamba mikono na miguu kabla ya kumuibia pesa

Mjukuu huyo wa kiume alimvuruta nyanyake kwenye chumba chake cha kulala kabla ya kumfunga kamba miguuni na mikononi kwa saa 6.

Muhtasari

• Mjukuu huyo alikuwa ameishi na nyanya yake kwa muda wa wiki tatu.

• Wanakijiji waliotaka kumchoma walimpiga vibaya lakini polisi wakafika kwa bahati nzuri na kumchukua hospitalini akisubiri kupona na kufunguliwa mashtaka.

Image: BBC

Ajuza wa miaka 66 amesimulia tukio la ajabu ambalo mjukuu wake wa kiume alimfanyia kkatika chumba chake cha kulala baada ya kuishi naye kwa muda wa wiki tatu.

Katika simulizi lililochapishwa na jarida la Nation, ajuza huyo alifika nyumbani kwake na kupata sanduku la mabati ambalo alikuwa ameweka pesa zake limevunjwa.

Kulikagua vizuri alipaka kiroba cha pesa alichokuwa ameweka ndani ya sanduku hilo hakipo pamoja na pesa zake elfu 2.

Alimuuliza mjukuu wake ambaye alikataa kutohusika katika kuchukua pesa hizo na kumtaka nyanya yake kuingia katika chumba chake cha kulala pamoja naye ili amsaidie kuzitafuta hela hizo.

Pindi tu walipofika kwenye chumba cha kulala cha nyanyake, mjukuu huyo mvulana kwa hasira alifunga mlango na kumvuruta nyanyake kitandani na kumtia Kamba katika mikono na miguu yake.

Alisokota kitambaa cha nguo mdomoni mwake ili kumzuia kupiga kelele na kuchukua kisu huku akianza kumtishia nyanya yake kwamba alitaka pesa Zaidi ili amfungue Kamba zile na kumuachia huru.

“Alikuwa akitetemeka. Aliniuliza ikiwa nitawaambia watu wengine kile kilichotokea, lakini nilimsihi ahifadhi maisha yangu, nikimhakikishia sitamwambiaa mtu yeyote. Aliendelea na kutishia kuniua ikiwa nitathubutu kufichua siri hiyo,” ajuza huyo alisimulia.

Baadae alimwacha nyanyake akiwa amemfunga Kamba, akaweka muziki kwa sauti ya juu na kuondoka ambapo alirudi saa moja baadae na ndizi tatu akimtaka nyanyake kula.

Kisha aliondoka tena na kumuacha nyanyake hapo katika hali hiyo ya Kamba – kwa Zaidi ya saa sita ambazo ajuza huyo alijaribu kujinasua.

“Baada ya kuhangaika sana, mwanamke huyo alifanikiwa kujifungua mwendo wa saa kumi jioni na mara akaruka dirishani, akiwaita majirani zake kuomba msaada. Kwa bahati nzuri, watoto wa jirani yake, wakija nyumbani kutoka shuleni, walisikia kilio chake na kuwajulisha wazazi wao waliokuja kumuokoa,” Nation waliripoti.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Rongai Wilberforce Sicharani alisema kijana huyo alikamatwa na majirani alipokuwa akirejea nyumbani.

Umati wa watu waliotaka kumuua, walimpiga mwanamume huyo kwa kipigo cha kutosha, na polisi wakamchukua akiwa amepoteza fahamu na kumpeleka katika hospitali ya Nakuru Level Five, anakopokea matibabu.