Mwanafunzi wa gredi 4 anauguza majeraha baada ya mwalimu kumchapa viboko 107

Mvulana huyo alikwenda ofisini kuripoti kuhusu kuibiwa kwa nguo zake bwenini, badala yake akashushiwa kipigo na mwalimu.

Muhtasari

• Mwanafunzi huyo alichapwa Jumapili iliyopita na walimu walipogundua ameumia vibaya, walimweka bwenini ili kuficha maovu yao na kumnyima matibabu.

Mwanafunzi auamia baada ya kuchapwa viboko 100
Mwanafunzi auamia baada ya kuchapwa viboko 100
Image: Kiss100

Mwalimu mmoja katika shule ya msingi ya Riang’ombe kaunti ya Nyamira anamulikwa na uchunguzi baada ya kudaiwa kumchapa mwanafunzi wa gredi 4 viboko Zaidi ya mia kwa mfululizo.

Kulingana na ripoti, Watumiaji wa Mitandao ya Kijamii wanaotumia lebo ya 'Haki kwa Mwanafunzi wa Darasa la 4' walidai kukamatwa mara moja na kufunguliwa mashtaka kwa mwalimu anayehusika kwa kukiuka sera ya Wizara ya Elimu kuhusu adhabu ya viboko.

Mwanafunzi huyo inasemekana alivamiwa Jumapili iliyopita na walipogundua kuwa majeraha yake ni makubwa, walimu wake walipanga njama ya kuficha tukio hilo kwa kumweka bwenini na kumnyima matibabu.

Jarida la Nation liliripoiti kwamba mjomba wa mtoto huyo wa kiume alidai mpwa wake alitiwa viboko vipatao 107 kwa mfululizo baada ya kwenda kuripoti kuhusu kuibiwa kwa nguo zake kutoka bwenini.

Mjomba alipokea simu kutoka kwa baba ya mtoto huyo ambaye alimjulisha kuhusu kitendo hicho baada ya kuarifiwa na mtoto mmoja, lakini juhudi zao za kufika shuleni ili kudhibitisha zilipata pingamizi kali kutoka kwa uongozi wa shule ambao haukuwa unataka mzazi yeyote kuruhusiwa kuingia, wakiwa wameweka ulinzi mkali kuzuia mtu wa nje kuingia.

"Walimjulisha kwamba mpwa wetu alipigwa vibaya na mwalimu ambaye alimpiga viboko 107 vya fimbo bila sababu za msingi,” mjomba huyo alidai kudokezewa na baadhi ya wanafunzi walioshuhudia tukio hilo.

Wanafunzi wa shule ya msingi wanadaiwa kumjulisha mjomba wa mvulana huyo kwamba mwanafunzi aliyejeruhiwa alikuwa amefua nguo zake na kuziacha zikauke. Hata hivyo, mtu alikwenda na kuchukua nguo.

Sasa wanamitandao wameungana na wanamitandao kuanzisha harakati za kutaka haki kutendeka, kwani ni hatia kwa mwanafunzi kuchapwa shuleni.