logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ndarugo: Gari la Avocado laanguka, siku 5 baada ya lori la mahindi na maharagwe kuanguka

Sehemu ya Ndarugo imekuwa gumzo baada ya kushuhudia ajali mara mbili kwa wiki.

image
na Davis Ojiambo

Habari31 March 2023 - 07:19

Muhtasari


  • • Ripoti mbalimbali zinaonyesha kuwa lori hilo lilipinduka kuzunguka Ndarugo - karibu na Juja, dakika chache baada ya saa 10 alfajiri.
Watu wakiiba avocado baada ya gari kuanguka

Kwa mara nyingine tena, wakaazi wa Ndarugo, katika barabara kuu ya Thika walijikuta katika hekaheka za hapa na pale kujizolea chakula baada ya gari lililokuwa likisafirisha avocado kuanguka sehemu hiyo.

Katika picha ambazo zilisambazwa mitandaoni Alhamisi, makumi ya watu walionekana waking’ang’ana kujizolea avocado hizo ambazo zilikuwa zimetapakaa barabarani baada ya ajali.

Hii inatokea siku tano tu baada ya lori lililokuwa likisafirisha shehena ya mahindi na maharagwe pia kupata ajali sehemu hiyo hiyo na mamia ya watu kufurika wakijizolea chakula hicho.

Usafiri katika barabara ya Thika, Jumamosi, Machi 25, ulitatizika baada ya lori hilo lililokuwa likisafirisha mahindi na maharagwe kupinduka kwenye barabara kuu yenye shughuli nyingi.

Ripoti mbalimbali zinaonyesha kuwa lori hilo lilipinduka kuzunguka Ndarugo - karibu na Juja, dakika chache baada ya saa 10 alfajiri.

Madereva wanaotumia barabara hiyo walirekodiwa wakipora mahindi na maharagwe kwenye mifuko ya guinea, kwani wengi wao waliweka mazao ya shambani kwenye magari yao kabla ya kuondoka.

Lori lililopinduka liliziba njia ya magari yaliyokuwa yakielekea Wilaya ya Biashara ya Nairobi (CBD).

Eneo la Ndarugo sasa limegeuka kuwa gumzo mitandaoni, baadhi wakizua utani kwamba Mungu anapenda watu wa eneo hilo kwani amekuwa akiwaletea vyakula kwa njia ya bwerere pasi na kutarajia, wakati huu ambapo maandanamo yanaendelea kote nchini kulalamikia gharama ya juu ya maisha na ugumu wa maisha.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved