Familia moja imezua mjadala mitandaoni baada ya kudaiwa kulikataa jeneza lililoletwa na mkwe kwa mazishi ya mama mkwe wake.
Kulingana na chapisho la utata ambalo lilichapishwa kwenye mtandao wa Facebook na Bem Raphael Aondongu, alisimulia kisa hicho akikiambatanisha na picha za jeneza husika, suala ambalo lilifungua milango kwa maoni mseto kutoka kwa wanamitandao.
Tukio hilo la ajabu lilijiri katika eneo la Tombo Mbatie, katika eneo la Serikali ya Mtaa wa Buruku Jimbo la Benue.
Kulingana naye, familia ilikataa jeneza hilo kwa sababu halikuwa zuri, na maskini sana kuweza kumzika mtu wa familia yao.
Aliandika, “Watoto wa mama aliyefariki walikataa na kutupa jeneza lililoletwa na mkwe kutoka kwa Wannue Tarkaa hadi kwa Tombo Mbatie, jimbo la Buruku BENUE. Alfajiri ya leo, familia isiyojulikana ilikataa sanduku lililoletwa na mkwe kwa ajili ya mazishi ya mama mkwe,” aliripoti.
Alizidi kueleza sa babu za mkwe kuleta jeneza na baadae kukataliwa akisema: “Kama mila ya TIV inavyodai, mama au baba anapofariki, mtoto wa kwanza wa kike ambaye ameolewa anatwikwa jukumu la kuandaa jeneza kwa ajili ya mazishi ya mzazi yeyote kati ya waliofariki. Na kwa ajili ya kudumisha mila, mtoto wa kwanza wa kike kwa kushirikiana na mumewe ambaye ni mkwe wa marehemu mama, walijaribu kwa kadri ya uwezo wao kuleta jeneza hili kwenye picha hapa chini lakini lilikataliwa.”
Kwa mujibu wa familia ya marehemu, walisema kuwa jeneza hilo si zuri na ni masikini wa kumzika mtu wa familia yao.