logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DJ Brownskin adaiwa kurekodi mkewe akifariki kwa kunywa sumu mbele ya watoto wake

Mkewe alianza kumtania kuwa angetaka kufa na kukoroga sumu kwa kikombe,

image
na Radio Jambo

Makala02 April 2023 - 08:17

Muhtasari


• Hata hivyo, video hiyo imezua mjadala mkali baadhi wakimtuhumu Brownskin kwa kutochukua hatua ya dharura.

• Wengine walisema hakuna kitu angefanya kwa mtu aliyeamua kujitoa uhai mwenyewe.

DJ Browskin amrekodi mkewe akifariki kwa sumu

Video yenye ukakasi ikionyesha jinsi mke wa DJ Brownskin alivyojitoa uhai kwa kunywa sumu imeibuka mitandaoni na kuzua hisia mseto.

Katika video hiyo ambayo inadaiwa kurekodiwa na Brownskin mwenyewe, inaanza pale ambapo mke wake anaonekana akikoroga mchanganyiko wa dawa zenye sumu kwenye kikombe.

Wakati huo wote mume wake, DJ Brownskin ako nyuma ya kamera na anadhaniwa kuwa ndiye anarekodi, huku mke wake akimwambia kuwa anataka kujiua.

Baada ya kukoroga sumu ile kwa kijiko kwa sekunde kadhaa za kuhesabika, mkewe anapiga funda moja zito la sumu na kutupa kikombe kando kisha kuketi kwenye kochi.

Dakika chache baadae anaanza kutokwa na pofu jingi mdomoni na kuwaambia watoto wake kuwa “nakufa wanangu” – lakini muda wote huu Brownskin haonekani kuchukua hatua yoyote ya dharura kujaribu kuokoa maisha ya mkewe, bali anaendelea kumrekodi akijigaragaza kwenye kochi kisha kuanguka sakafuni.

Baada ya kuanguka sakafuni, Brownskin anamuita msichana mmoja - anayedhaniwa kuwa mjakazi - aliyefika kwenye sebule na kumtaka kumpa maziwa.

“Kuna maziwa, hebu mpe maziwa, mlazimishie akunywe,” Brownskin anasikika akimwambia msichana yule.

Hata hivyo, mkewe wakati huu anaonekana kulemewa kabisa na sumu na yuko sakafuni anajigaragaza kutokana na makali ya sumu mwilini, hawezi hata kushika kikombe cha maziwa na msichana yule anaonekana kuchanganyikiwa hajui cha kufanya.

Msichana anajaribu kumlazimishia mdomoni na wakati huu watoto wake wadogo wanafika na kumuuliza baba yao ni nini kimetokea kwa mama yao.

Brownskin ambaye haonekani kushtushwa na kitendo hicho anamwambia mtoto mmoja “patia mama maziwa”.

Mkewe anang’ang’ana mwenyewe sakafuni hadi kuzima kabisa na video hiyo imezua maoni kinzani kwenye mitandao ya kijamii, baadhi wakimtuhumu Brownskin kwa kuangalia mkewe akijitoa uhai bila kuchukua hatua yoyote na wengine wakisema hakuna kitu angefanya kumsaidia mtu ameamua kujitoa uhai.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved