logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Video ya Mama akimchinja mwanawe wa miaka 2 na kula matumbo, figo yazua ghadhabu

Inaarifiwa alifanya hivyo baada ya kukosana na baba mtoto wake.

image
na Radio Jambo

Habari25 April 2023 - 04:33

Muhtasari


• Ripoti ya polisi inaeleza kuwa mwanamke huyo alimkata mtoto wake vipande vipande kabla ya kumla utumbo na figo.

Mwanamke mjamzito apatikana amedungwa visu mgongoni

Video ya mwanamke akimchinja kinyama mwanawe wa miaka miwili na baadae kuanza kula baadhi ya viungo vya mwili wake imevutia hisia kinzani kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya video hiyo kusambaa, makachero kutoka idara ya DCI eneo la Kitengela kaunti ya Kajiado walimweka chini ya ulinzi mama huyo wa miaka 27 ambaye alirekodiwa akiwa amejifungia ndani ya nyumba yake.

Majirani na mashuhuda walifuatilia tukio hilo bila uwezo wa kutoa msaada kwa mtoto huyo kupitia kwa dirisha kwani alikuwa amejifungia.

Inaarifiwa Olivia Naserian alichukua uamuzi huo baada ya kuachana na baba mtoto huyo.

Ripoti ya polisi inaeleza kuwa mwanamke huyo alimkata mtoto wake vipande vipande kabla ya kumla utumbo na figo, katika kisa kilichowaacha vinywa wazi wenyeji kwa hasira.

Naseren alikuwa amejifungia ndani ya nyumba yake akicheza na mtoto huyo alipopata jeuri ghafla na kuanza kuvunja vitu vya nyumbani.

Kelele hizo ziliwavutia majirani zake ambao walitazama kwa kutoamini akimshukia bintiye kwa kisu zaidi ya mara 100, kwani hawakuweza kuingia kwenye chumba hicho kuokoa roho isiyo na hatia.

"Mtoto mwenye umri wa miaka miwili alikatwakatwa na mamake vipande vipande, na baadaye alilazwa matumbo yake mshukiwa alipatikana katika eneo la tukio akiwa amepoteza fahamu na kusindikizwa katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Kitengela kwa matibabu," ripoti ya polisi ilisoma kwa sehemu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved