Fahamu mali inayomilikiwa na aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko

Utajiri huu umewafanya wakenya wengi kutaka kujua jinsi Sonko alipata utajiri wake.

Muhtasari

• Utajiri huu umewafanya wakenya wengi kuwa na hamu ya kufahamu mali anazomiliki Sonko na jinsi Sonko alipata utajiri wake.

• Anamiliki pia majumba makubwa katika kaunti mbalimbali nchini.

Sonko aonesha kiburi cha pesa Twitter
Sonko aonesha kiburi cha pesa Twitter
Image: Twitter

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ameibua mjadala mtandaoini baada ya kuchapisha video inayoonyesha utajiri wake mnono.

Katika video hiyo, mwanasiasa huyo anaonekana akifungua masanduku makubwa yaliyojaa pesa nyingi za kigeni huku akimpigia simu mtu fulani kwa kutilia shaka utajiri wake.

Utajiri huu umewafanya wakenya wengi kuwa na hamu ya kufahamu mali anazomiliki Sonko na jinsi Sonko alipata utajiri wake.

Awali Sonko akizungumza na runinga moja nchini alihusisha himaya yake, ambayo anasema inaanzia kwenye majumba ya kukodisha hadi kwa magari miongoni mwa nyingine, kama faida ya uwekezaji aliofanya awali maishani.

Sonko ambaye pia alikuwa Mbunge wa Makadara, seneta na kisha gavana alidai kwa bashasha kuwa anamiliki mali ya zaidi ya bilioni 20.

“Ninamiliki mali kutoka Lamu hadi Vanga. Nina hati miliki zaidi ya 1000 za ardhi na magari… nina hati ya umiliki zaidi ya magari 150 ambayo ninamiliki,” alisema.

Mwanasiasa huyo pia anamiliki vilabu kadha vya burudani a nchini na hivi majuzi alifungua klabu moja kubwa eneo la Shanzu VIP Volume Club mjini Mombasa.

Awali kabla ya kuwa mbunge wa Makadara alikuwa anamiliki matatu jijini Nairobi kwa ushirikiano na mkewe Primrose Mbuvi.

Anamiliki pia majumba makubwa katika kaunti mbalimbali nchini.