Whatsapp yakubali watumizi kuficha jumbe za siri

WhatsApp imefanya mabadiliko na sasa waweza kuficha mazungumzo au jumbe.

Muhtasari

• Mabadiliko haya yalitangazwa na mmiliki wa mtandao huo Mack Zuckerberg katika akaunti yake ya facebook.

• Mabadiliko haya yatawaruhusu watumiaji wa whatsapp kuweza kuzificha jumbe ambazo hawataki kujulikana kwenye folda yenye neno siri.

Kampuni ya mawasalinao ya Whatsapp imefanya mabadiliko na sasa unaweza kumkabali mtu kuficha mazungumzo au jumbe.

Mabadiliko haya yatawaruhusu watumiaji wa whatsapp kuzificha jumbe ambazo hawataki kujulikana kwenye folda yenye neno siri.

Mfuko huo wa siri hautaonyesha notisi ya ujumbe kuingia kama ilivyo kawaida ya jumbe za kawaida ili kuarifu mtumiaji kuwa kuna ujumbe mpya.

Mabadiliko haya yalitangazwa na mmiliki wa mtandao huo Mack Zuckerberg katika akaunti yake ya facebook.

Image: MARK ZUCKERBERG

Mabadiliko haya yanajiri baada ya mabadiliko kadhaa kutangazwa na Zuckerbarg hivi majuzi.

Pia mtandao huo pia sasa unawaruhusu watumiaji kuchapisha sauti katika status zao za whatsapp.

Watumiaji pia wanaweza kutoa hisia zao badala ya kuandika majibu (kulia, kicheko, kulia, kupenda moyo, kushtuka na kuomba).