Mbunge Babu Owino na mbunge Peter Salasya walimana mitandaoni

Huku akiikosoa ripoti hiyo ya Politrack Africa, Salasya amedai imefadhiliwa na Babu Owino.

Muhtasari
  • Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro aliorodheshwa kidedea – bora zaidi kwa asilimia 73.7 kulingana na ripoti ya Politrack Africa, huku Patrick Makau (Machakos) akiwa wa tatu (70.6).
MBUNGE PETER SALASYA
Image: HISANI

Vita vya maneno kati ya mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino na mwenzake wa Mumias Mashariki, Peter Salasya vimeshuhudiwa mitandaoni kufuatia ripoti ya hivi punde ya rekodi ya utendakazi.

Vita hivyo vimeibuka  kutokana na ripoti hiyo, inayomuorodhesha Babu Owino kama mmoja wa wabunge wanaoongoza katika utendakazi wa maeneobunge nchini.

Huku akiikosoa ripoti hiyo ya Politrack Africa, Salasya amedai imefadhiliwa na Babu Owino.

Salasya, anayehudumu kipindi cha kwanza bungeni anaamini anafanya bora zaidi.

Akiandka na kutoa madai hayo kupiria kwenye akaunti yake rasmi ya twitter mbnge huyo alisema;

“Ripoti ya Politrack Africa ni uongo mtupu, hata katika Twitter akaunti yangu ina wafuasi wengi kuliko yao. Mfadhili wao ni Babu Owino, ambaye ni miongoni mwa wafuasi wachache wanaowafuata. Mara hii tumewashika,” Salasya alisema.

“Ninaamini nimefanya kazi bora nyanjani na ninakua kisiasa, na hata wao wanajua hivyo ndio maana wananunua kampuni kutoa ripoti ghushi ya utendakazi kujaribu kunitisha. Nina malengo makuu."

Mbunge  Babu Owino, ameorodheshwa mbunge wa pili bora nchini akipewa asilimia 72.1.

Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro aliorodheshwa kidedea – bora zaidi kwa asilimia 73.7 kulingana na ripoti ya Politrack Africa, huku Patrick Makau (Machakos) akiwa wa tatu (70.6).

Akimjibu Salasya, Babu Owino aliandika katika ukurasa wake rasmi wa twitter: “Mheshimiwa Peter Kalerwa Salasya, Politrack iliorodhesha wabunge kwa mujibu wa utendakazi wao ila sio kwa uwendawazimu. Ulichaguliwa kufanyia wananchi kazi, ila si kuwa mcheshi wa kijijini na mwendawazimu…”

 

Mbunge huyo wa chama cha ODM, pia anaongoza katika orodha ya wabunge kiwango cha kaunti, Nairobi.

Licha ya maneno makali ambayo wawili hao wamerushiana,bila shaka wabunge hao ni wafuasi sugu wa kinara wa ODM Raila Odinga.

Pia walionekana wakiwa mstari wa mbele katika maandamano wa Azimio ya kupinga Serikali kuu wiki zilizopita