Jeff alinifurahisha kwa sababu ya uhusiano wa karibu na mama yake

Msanii wa Mugithi DJ Fatxo kwa mara ya kwanza amezungumza kwa njia ya kipekee kuhusu sakata katika kifo cha Jeff Mwathi.

Muhtasari

• Mwanamziki huyo alisema ilimlazimu kutembea na Jeff kwa gari yake baada ya kumwalika nyumbani kwake na alipaswa kutembea  kuenda kuona wanabiashara walio kuwa wakimpa kazi.

• Mwanamziki huyo alisema ilimlazimu kutembea na Jeff kwa gari yake baada ya kumwalika nyumbani kwake na alipaswa kutembea  kuenda kuona wanabiashara walio kuwa wakimpa kazi.

DJ Faxto anayeshukiwa kwa kifo cha Mwathi
DJ Faxto anayeshukiwa kwa kifo cha Mwathi
Image: HISANI

Msanii wa Mugithi DJ Fatxo kwa mara ya kwanza amezungumza kwa njia ya kipekee kuhusu sakata ambalo limekuwa likimuandama katika kifo cha aliyekuwa mbunifu wa mapambo Jeff Mwathi.

Fatxo akizungumza katika kipindi cha Radio Jambo na mtangazaji Massawe Japanni, alisema kuwa marehemu alikua na uhusiano wa karibu na mama yake na ndio maana alimfurahisha.

Katika ya kifo cha Jeff, Dj Faxto alisema walikua pamoja kwa sababu alikua na nia ya kumuajiri kufanya mapambo ya ndani katika biashara yake aliyokuwa akitaka kufugua baada ya kufanya ukarabati kwa maduka hio.

Mwanamziki huyo alisema ilimlazimu kutembea na Jeff kwa gari yake baada ya kumwalika nyumbani kwake na alipaswa kutembea  kuenda kuona wanabiashara walio kuwa wakimpa kazi.

Dj Faxto alisema kuwa mbunifu huyo wa mapambo alikua anazungumza na mama yake na kumuarifu kila pahali ambapo walikua wakienda,

"Jeff alikua anazungumza na mama yake kuhusu kila mahali tulikua tunaenda kupitia voice note kwa mtanadao wa mawasiliano wa whatsapp."  Faxto alisema.

Faxto alisema kuwa mahusiano haya ya karibu ya Jeff na mama yake ilimmfurahisha sana kwani yeye alikua na uhusiano uliokua ukilandana na huo wa jeff na mama yake.

"Mimi na mama yangu tuko karibu hivyo hivyo, mimi ata kabla ya kuanza shoo huwa nazungumza na mama yangu." Faxto aliongeza.

Mwanamziki huyo alisema ilimlazimu kutembea na Jeff kwa gari yake baada ya kumwalika nyumbani kwake na alipaswa kutembea  kuenda kuona wanabiashara walio kuwa wakimpa kazi.

"Kwa hivyo baada ya kuona mtu mwenye uhusiano na amama yake nilifurahishwa na yeye."