Jubilee ni mzigo kwa Azimio-MCA Alai adai

Viongozi wa jubilee walikutana Jumatatu huku viongozi kutoka vyama vingine vya kisiasa walijiunga nao.

Muhtasari
  • Kulingana na Alai, Jubilee inazidi kuwa mzigo mkubwa kwa Azimio haswa ikizingatiwa Uhuru Kenyatta amebanwa na washirika wa Kanini Kega.
Alai asuta makampuni ya kamari kupeleka wachekeshaji Qatar
Alai asuta makampuni ya kamari kupeleka wachekeshaji Qatar
Image: Facebook

MCA wa Wadi ya Kileleshwa Robert Alai ametaja chama cha jubilee kuwa dhaifu na kuchanganyikiwa kutoka juu hadi chini.

Kulingana na Alai, Jubilee inazidi kuwa mzigo mkubwa kwa Azimio haswa ikizingatiwa Uhuru Kenyatta amebanwa na washirika wa Kanini Kega.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter Alai alisema;

"Lakini Jubilee ni mzigo mzito kwa Azimio sasa.Ni haki tu kwamba wanapanga fujo zao na kisha kualikwa kurudi,Uongozi wa bunge unapaswa kugawanywa kati ya ODM na vyama vingine vya Azimio lakini sio Jubilee.

Uongozi wa Jubilee unaonekana kuwa dhaifu na wenye kuchanganyikiwa. Waache waweke utaratibu wa nyumba yao."

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa Ann Nderitu tayari imethibitisha kuwa kongamano la kitaifa la wajumbe wa Jubilee lililofanyika siku ya Jumatatu lilikuwa batili.

Hii inamaanisha kuwa Kanini Kega ndiye Katibu Mkuu wa chama cha jubilee na Sabina Chege kiongozi wa chama.

Rais wa zamani Uhuru Kenyatta aliweka wazi siku yab Jumatatu jana kuwa yeye ndiye kiongozi wa chama cha jubilee na hatatishwa.

Hata hivyo, ni wazi kuwa Uhuru na muungano mzima wa Azimio wamewekwa kwenye kisanduku ambapo wanajikuta wakibanwa vibaya.

Viongozi wa jubilee walikutana Jumatatu huku viongozi kutoka vyama vingine vya kisiasa walijiunga nao.

Viongozi hao walionekana kuikosoa Serikali ya Kenya Kwanza kwa gharama ya juu ya maisha,huku wakidai kuwa sio waasi ambao wanataka kubomoa chama cha Jubilee ilhali ni Rais Ruto.

Uhuru alitumia fursa hiyo kukabiliana na wakosoaji wake vilivyo,huku akisema kwamba hatatishwa ili aweze kustaafu kutoka kwa siasa.

Ni dhahiri kuwa jubilee imepoteza mwelekeo na hakuna uwezekano kuwa Uhuru atafaulu katika juhudi zake za kusalia kisiasa.