Nilipima DNA kimzaha na kugundua mtoto nimelea kwa miaka 12 si wangu - Mama alia

"Baada ya miaka 12 tulipogundua tulichanganyikiwa. Tuliamua kumwambia mtoto ukweli. Tulipompasulia mbarika, alituangalia kwa sekunde kadhaa kisha akasema "nawapenda pia".

Muhtasari

• “Kusoma matokeo ya kipimo cha DNA mtandaoni, niliona kuwa kulikuwa na makosa." - Mama huyo alisema.

Mama apima DNA baada ya miaka 12 na kugundua mtoto si wake
Mama apima DNA baada ya miaka 12 na kugundua mtoto si wake
Image: SUN

Mwanamke mmoja kutoka nchini Marekani ni mwingi wa mawazo mtanange baada ya kupima DNA kwa kujifurahisha tu na kupigwa na butwaa alipogundua mtoto ambaye amekuwa akilea kama wake kwa miaka 12 si wake.

Kulingana na jarida la The Sun, Donna Johnson mwenye umri wa miaka 47 hakuwa anadhamiria kupatana na mshtuko wa aina hiyo kwani alikuwa anafanya vipimo vya DNA kwa mwanawe kimzaha tu.

“Kusoma matokeo ya kipimo cha DNA mtandaoni, niliona kuwa kulikuwa na makosa. Walisema kwamba mume wangu Vanner, ambaye sasa ana umri wa miaka 47, alikuwa baba ya mwana wetu mkubwa, lakini baba na mama wa mdogo wetu hakujulikana,” Johnson aliambia jarida hilo baina ya kwikwi.

“Nilijaribu sana kuelewa. Kisha, katika wakati wa uwazi wa kuudhi, niligundua lazima kulikuwa na mchanganyiko kwenye kliniki ambapo tulikuwa na IVF (utaalam wa kisayansi ambapo yai la mwanamke hutolewa na kutiwa mbegu ya kiume kwenye maabara). Nilikutana na Vanner, ambaye anafanya kazi katika programu ya fedha, katika shule ya upili,” aliongeza.

Wanadoa hao walioana mwaka 2003 na kupata mtoto wao wa kwanza ambaye ana miaka 18 lakini wakapata matatizo wakati wa kujaribu kutafuta mtoto wa pili.

Hapo ndipo waliamua kutafuta huduma za utaalam wa IVF mwaka 2007.

“Mnamo Machi 2007, tulikuwa na mzunguko wetu wa kwanza wa IVF kwa kutumia mayai yangu na manii yake. Ilishindikana, lakini majira hayo ya joto, tulijaribu tena na ilifanya kazi. Wakati mwana wetu Tim alizaliwa mnamo Agosti 2008, ilionekana kama muujiza. Kama ndugu wengi, wavulana walikuwa tofauti,” mama alieleza.

Mtoto huyo alikuja kuwa si wake, baada ya miaka 12 y malezi akijua kuwa ni damu yake.

“Kwa usaidizi wa mshauri, tuliishughulikia na tukaamua kumwambia Tim - wakati huo akiwa na umri wa miaka 12 - ukweli, tukifikiri itakuwa mbaya zaidi ikiwa angejua kama mtu mzima. Alikuwa kimya sana na akasema anatupenda sisi pia.”