"Nimemiss maandamano" - Babu Owino

Mbunge huyo alisema kuwa anatamani maandamano hayo yarudi hivi karibuni.

Muhtasari

• Pia alimpongeza mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro kwa kuorodheshwa kama mbunge bora nchini.

• Katika mahajiano na mwanablogu Vincent Mboya, Babu Owino alisema kuwa anazikosa Teargas na anatamani warudi kugoma.

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino
Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino
Image: INSTAGRAM

Mbunge wa Embakasi Mashariki Paul Ongili Owino almaruufu Babu Owino amesema  kuwa anakosa maandamano sana na kuwa angependa muungano wa Azimio urejelee maandamano hayo.

Katika mahajiano na mwanablogu Vincent Mboya, Babu Owino alisema kuwa anazikosa Teargas na anatamani warudi kugoma.

"Nakosa maandamano sana, nasema tu ukweli nakosa sana teargas, ata sasa niko na homa na kama kungekua na maandamano ningekula teargas na nihisi nafuu," alisema Babu Owino.

Mbunge huyo chipukizi aliongeza kuwa anatamani maandamano hayo yarudi hivi karibuni akisema kuwa chanzo kikuu cha kutaka maandamano yarejee ni kwa sababu ya hali ya juu ya maisha.

"Hali ya juu ya maisha na ushuru unaongezwa na serikali na pesa wanazoenda nazo nyumbani ni nyingi kuliko ushuru wanazokusanya."

Alipoulizwa maandamano hayo yalikua yakitaka kuafikia nini, Babu Owino alijibu kuwa wanatarajia bei ya bidhaa muhimu kushuka, kuhakikisha kuwa tume ya uchaguzi ya IEBC imundwa ipasavyo na kuzipigania haki za Wakenya.

Wiki iliyopita mbunge huyo alioreodheshwa namba mbili kwa wabunge wachapa kazi bora nchini, na aliwashukuru shirika la Politrack Africa kwa kutambua kazi yake kwa wakazi wa Embakasi Mashariki.

Nina furaha sana kuweza kuorodheshwa namba mbili kwa wabunge wanaofanya kazi bora nchini Kenya. Kuoredheshwa huko kunahitaji kazi mingi na kwa kweli nadani ya eno la Embakasi Mashariki tumekua tukifanya akzi kwa kweli,"

Pia alimpongeza mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro kwa kuorodheshwa kama mbunge bora nchini.