Daktari aamrishwa kulipia malezi ya mtoto baada vasektomi kufeli

Daktari huyo anatarajiwa kulipa msaada wa mtoto hadi afikishe miaka 18.

Muhtasari

• Shtaka hilo limekuwa mahakamani kwa miaka mingi na hatimaye kuamuliwa huku mtoto huyo akifikisha umri wa miaka 10.

• Licha ya kuhakikishiwa utaratibu huo ulifanikiwa mwaka 2013 mke wa mtu huyo alijifungua mtoto wa tatu.

Wataalam wa upasuaji katika chumba cha upasuaji wakimshughulikia mgonjwa
Wataalam wa upasuaji katika chumba cha upasuaji wakimshughulikia mgonjwa
Image: MAKTABA

Daktari mmoja kutoka Colombia ameagizwa kulipa pesa za kusaidia kulea mtoto wa mgonjwa wake baada ya vasektomi aliyomfanyia mwanaume huyo kufeli.

Daktari huyo anatarajiwa kulipa msaada wa kumlea mtoto huyo hadi atakapofikisha umri wa miaka 18.

Kulingana na news.com.au wazazi wa mtoto huyo, ambao tayari walikuwa na watoto wawili, waliamua kufanya vasektomi mwaka wa 2012 baada ya kupata watoto wawili.

Wakitaja ugumu wa kifedha kutokana na baba huyo kukabiliwa na tatizo la upotevu wa kusikia jambo ambalo linadaiwa kuwafanya kupata kazi kuwa ngumu, wanandoa hao walimtafuta daktari wa upasuaji ili kumfanyia upasuaji huo wa kawaida.

Licha ya kuhakikishiwa utaratibu huo ulifanikiwa mwaka 2013 mke wa mtu huyo alijifungua mtoto wa tatu.

Shtaka hilo limekuwa mahakamani kwa miaka mingi na hatimaye kuamuliwa huku mtoto huyo akifikisha umri wa miaka 10.

Binti huyo atakapofikisha umri wa miaka 18, daktari anatarajiwa kuwa amelipa peso za Colombia milioni 295 (takriban milioni 9,071,922 pesa za Kenya).

Wiki zilizopita mwanamume mmoja wa Kakamega alisema alikuwa mjamzito licha ya yeye kufanya vasektomi.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 36 ambaye alifanyiwa upasuaji wa vasektomi kwa hiari mwaka wa 2022, aliashangazwa na habari kutoka kwa mkewe kuwa ni mjamzito.

Mwanamume huyo kutoka Kakamega akizungumza na runinga ya Citizen alisema kuwa alikubaliana na mkewe kufanyiwaa upasuaji huo baada ya kupata watoto watatu.

Kulingana nay eye alijitolea kufanya vasektomi kwa sababu alihisi wanawake wanabeba mzigo mkubwa katika juhudu za upangaji uzazi.