KUTOA USHURU TUTAJITEGEMEA

Lazima tukusanye ushuru - Gachagua

Wakenya wanaendelea kufurahia huduma za serikli na hakuna kuhangaishwa

Muhtasari

• Jinsi ya kuendesha uchumi mbele si kuongeza madeni bali ni kupitia kuyazalisha mapato yetu sisi wenyewe.


Naibu rais Rigathi Gachagua
Image: FB// DP RIGATHI GACHAGUA

Naibu wa rais Rigathi Gachagua kwa mara nyingine amesisitiza hoja ya rais Ruto kukusanya ushuru.

Gachagua alisema hili wakati alipoandamana na rais Ruto katika makao makuu ya Mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini Kenya (KRA) mjini Nairobi kwa shughuli ya kuthibitisiha makato yake ya ushuru kabla ya zoezi yo kukamilika mwezi Juni.

Alipokuwa akimkaribisha rais kuzungumza Gachagua alisema kuwa,jinsi ya kuendeleza taifa si kwa kuomba bali ni kwa kuzalisha mapato yetu wenyewe na kutumia maliasili yetu ipasavyo. “ Mheshimiwa rais, nina furaha kubwa kila nikiandama  nawe kufanikisha miradi ya maendeleo na kubadilisha suala la uchumi katika taifa letu.” Gachagua alitanguliza.Aliendelea na kusema kuwa,“ Ningependa kukutia moyo kwamba tupo katika njia inayofaa katika maendeleo, watu wametulia hivi kwamba mipango ya kuchukua madeni inaendelea kufifia. Jinsi ya kuendesha uchumi mbele si kuongeza madeni bali ni kupitia kuyazalisha mapato yetu sisi wenyewe.”

Mpango unaondelea wa ushuru wa nyumba, kwa madai ya Rais Ruto ni kwamba, mbali na kuwatafutia wanaoishi vibamdani nyumba nzuri tena za bei nafuu,kutachipuka pia nafasi za ajira kwa Wakenya  wengi ambao asilimia kubwa kwa sasa haina kazi.  

“Lazima tufunike mashimo yote yanayovuja ushuru ndipo kupata pesa za kutosha kufanikisha miradi ya maendeleo kwa watu wa Kenya. Hatutumii njia ya kukusanya ushuru ndipo kuwanyanyasa waliotupinga kisiasa,masala ya ushuru ni ya ushuru na yale ya kisiasa yatashughulikiwa kisiasa hakuna siku tutawauliza maafisa wa KRA watusaidie kupambana na wapinzani,kazi ya KRA ni kukusanya ushuru na kuhakikisha uwazi na uwajibikaji wa ushuru huo.”  Gachagua aliendelea. Aliendelea kwa kukiri kwamba inadhihirika kwamba Wakenya wanafuruahia huduma za serikali na uongozi wake hakuna kutishiwa wala kuhangaishwa.