AREJELEWA KAMA ZAKAYO

Zakayo Mtoza ushuru – Rais Ruto akubali jina jipya la majazi

Kwa kuwa wamenirejelea kama Zakayo,tutaliangazia hilo

Muhtasari

•Tunayo siku ya watoa ushuru,pendekezo langu ni kuwa,tunaweza kuwa na siku ya wakusanyaji ushuru labda katika ikulu.

•Kwa kuwa nimerejelewa kama Zakayo katika baadhi ya maeneo,hili ni pendekezo zuri na tutaliangazia

Rais William Ruto
Rais William Ruto
Image: Facebook

Rais William Ruto amekiri kwamba tayari raia wamembandika jina Zakayo mtoza ushuru.

Hili limebainika katika jumba la Times Tower alipokuwa akizungumzia  kuhusu namna  ya kuendesha taifa mbele kutokana na ushuru.Ruto alipokuwa akihutubia umati, alilisema hilo alipoulizwa iwapo kuna uwezekano wa kuwepo kwa siku ya wakusanyaji ushuru swali lilioulizwa na mmoja wa maafisa wa KRA.

“Tunayo siku ya watoa ushuru,pendekezo langu ni kuwa,tunaweza kuwa na siku ya wakusanyaji ushuru labda katika ikulu?” Muila aliuliza.

Ruto alimjibu kuwa, tayari amekwisha kuwekwa jina Zakayo katika baadhi ya maeneo, hilo ni pendekezo zuri na hivyo serikali italitilia maanani.

“Kwa kuwa nimebandikwa jina Zakayo katika baadhi ya maeneo,hili ni pendekezo zuri na tutaliangazia.”Ruto alimjibu.

“Tutaendelea kutafuta  njia ambazo ushuru utakusanywa kwa uadilifu kuhakikisha hakuna kuvuja.” Rais aliendelea.

Haya yanajiri huku wakenya wakipitia hali ngumu ya maisha kutokana na bei ghali ya bidhaa muhimu za matumizi. Shirika la mafuta nchini limekuwa la punde kutangaza kupandishwa kwa bidhaa hiyo huku nayo kampuni ya  umeme na kawi ikiendelea  kupandisha bei ya huduma hizo bila kuzungumzia bei ya sukali ambayo kwa sasa ni maradufu.

Rais ambaye anapigia debe kuwepo kwa ushuru ili kufanikisha ujenzi wa nyumba, alieleza bayana kuwa nia yake ni kuhakikisha wakenya wapepata makao mazuri tena ya bei nafuu ili wanaoishi vibandani pia wanufaike.

Ruto pia aliendelea na kusema kwamba, cha muhimu ni kuhakikisha kwamba ushuru unaotozwa wananchi unatumika kwa njia ambayo inakusudiwa na ataendeleza uwazi kuukomesha ufisadi na uvujaji wa mali ya umma na hivyo Wakenya wamwuunge mkono.

“Itatarajiwa kuwa gharama ya maisha itakuwa juu,maana nasikia sina pesa ya za kununua baadhi ya bidhaa,lakini licha ya hayo lazima pia taifa lisonge mbele.Hili litafanyika kupitia ushuru kutoka kwetu sisi Wakenya.” Ruto alieleza hoja ya teknolojia katika taifa.