Tasnia ya riadha nchini Kenya wanaomboleza kifo cha mwanariadha Sammy Kosgei aliyegongwa na gari katika eneo la Kapseret kaunti ya Nandi, kulingana na jarida la Nation.
Jarida hilo linaripiti kwamba Kosgei aligongwa na gari la uchukuzi wa umma ambalo lilitoroka baada ya kutekeleza maovu hayo Ijumaa jioni.
Ripoti ya polisi ilionyesha kuwa mshikilizi huyo wa zamani wa rekodi ya dunia zaidi ya kilomita 25 aligongwa na gari lililokuwa likienda kasi na kufariki papo hapo.
Kamishna wa Polisi wa Kaunti ya Nandi Joseph Kavoo alisema mwanariadha huyo alikuwa akitembea-tembea kwenye barabara kuu ya Lessos-Kapsabet gari lililokuwa likienda kasi lilipomgonga kabla ya kuondoka kwa kasi.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Emeki mwendo was aa moja na nusu usiku na kwamba gari hilo halikusimama bali lilifululiza mbio kuondoka baada ya kusababisha ajali hiyo.
Kosgei alivunja rekodi ya mbio katika makala ya 43 ya mbio za Barcelona Marathon mnamo 2021, na kurekodi muda wa 2:06.04 ambao uliwekwa mnamo 2019 na Alemu Bekele