logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wacheni kutuma watoto nyumbani kuendea chakula - MP Barasa awasihi walimu

Kuna baadhi ya walimu hapa hawana hayo maharagwe,watoto watatoa wapi?

image
na

Makala29 May 2023 - 08:46

Muhtasari


•Barasa ametoa wito kwa walimu wakome kuwafukuza watoto katika shule za msingi ili kuendea mahindi na maharagwe.

•Barasa pia alionya walimu dhidi ya kujitungia sheria zisizo katika katiba, kuwafukuza watoto darasani kwa madai ya kuleta chakula.

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa ametoa wito kwa walimu wakome kuwafukuza watoto katika shule za msingi ili kuendea mahindi na maharagwe.

Barasa alisema hayo wakati alipohudhuria hafla katika kaunti ya Bungoma alipokuwa ambapo aliezea hali inayowakabili wazazi hasa wakati huu taifa lipo katika hali mbaya kiuchumi. 

“Nilipokuwa naenda nyumbani,nilikutana na wanafunzi wengi shule nzima wakiendea nyumbani.Nilipowauliza wanaenda wapi waliniambia wameambiwa waende walete maharagwe goro goro mbili.” Barasa alisema alipokuwa akihutubia umati.

Kiongozi huyo ambaye alichaguliwa kwa mara ya pili kupitia tikiti ya UDA  Kimilili, alibainisha kwamba kwa sasa taifa limekumbwa na hali ngumu ya maisha na kuwatania walimu kwamba pia baadhi yao hawana maharagwe kwao.

“ Maharagwe saa hii yamepanda, gorogoro  moja saa hii ni 600, kuna baadhi ya walimu hapa hawana hayo maharagwe. Kuna mzee mmoja jirani yangu ambaye ana watoto 6 wa wasichana wake.Kila mtoto akileta gorogoro mbili mbili mara sita kisha mara 600, huyo mzee atatoa pesa hizo zote wapi? Hii pesa ni nyingi kwa mzazi na kila mzazi anajua kile ambacho mtoto wake atakula.” Aliongeza.

Barasa pia alionya walimu dhidi ya kujitungia sheria zisizo katika katiba, kuwafukuza watoto darasani kwa madai ya kuleta chakula.“

"Wacheni kuwatuma watoto nyumbani ovyoovyo,wacha watoto wakae darasani wasome,wapite mitihani wawe gavana ndipo waje kusaidia Bungoma.”

Haya yanajiri wakati ambapo bei ghali ya bidhaa muhimu hasa bidhaa za matumizi ya kila siku zikiendelea kuibua mijadala kila kuchao miongoni mwa Wakenya wakisihi serikali itilie maanani mtakwa yao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved