Nilifumania babangu na mke wangu wakifanya mapenzi, sasa wanatarajia mapacha!

Mwanamume huyo ambaye anafanya kazi ya kuhudumia maiti mochwari alisema alikuwa anachungulia kifaa cha kurekodi alichokibandikiza nyuma ya mlango wa baba yake.

Muhtasari

• Darren - ambaye alikataa kutoa maoni - atakuwa babu na baba wa kambo wa Willow ikiwa ataoa Stephanie.

• Watoto wa Stephanie watakuwa kaka au dada wa kambo wa Declan na kaka au dada wa kambo wa Willow na pia shangazi au mjomba wake.

 

Mwanamume mwenye huzuni na mfadhaiko.
Mwanamume mwenye huzuni na mfadhaiko.
Image: Maktaba

Mfanyikazi wa mochwari anasema alitengana na mkewe baada ya kumkamata akishiriki mapenzi na babake - na wanandoa hao sasa wanatarajia mapacha.

Kwa mujibu jarida la The Sun, Declan Fuller, kutoka Rhondda huko South Wales, anadai kuwa alimwona ex wake, Stephanie, pia 22, akiingia chumbani na baba yake mwenye umri wa miaka 44, Darren.

Alipomuuliza Stephanie kilichotokea alisema: 'Tulikuwa tunatazama The Simpsons kwenye TV.'

Darren na Stephanie - ambaye sasa ni mjamzito - wanaishi pamoja karibu maili sita mbali na nyumba ya aliyekuwa mume wake, Fuller.

Lakini Stephanie anasisitiza kuwa hakuwa mwaminifu kwa mpenzi wake wa zamani, akiambia The Sun: 'Sikumsaliti Declan. Tulikutana wiki moja au zaidi baada ya kuniacha.'

Declan alisema: 'Ni kama njama. Sio kawaida. Ninahisi kusalitiwa lakini niko vizuri zaidi bila wao wawili.'

Mume huyo mchanga alitilia shaka baada ya Darren, ambaye ametalikiana, kuhamia naye, Stephanie na binti yao Willow mwenye umri wa miaka miwili Septemba iliyopita.

Miezi miwili baadaye aliangalia kifaa cha kufuatilia mtoto, ambacho alikuwa amebandikiza kwenye mlango wa baba yake.

Watoto wa Stephanie watakuwa kaka au dada wa kambo wa Declan na kaka au dada wa kambo wa Willow na pia shangazi au mjomba wake.

Darren - ambaye alikataa kutoa maoni - atakuwa babu na baba wa kambo wa Willow ikiwa ataoa Stephanie.

Katika taarifa zinazoambatana na hizo, Jumatatu Radio Jambo ilisimulia tukio moja ambalo lilijiri kwenye nyumba ya wageni ambapo mwanamume alikwenda kwenye loji hiyo akiwa na mpango wake wa kando na kumfumania mke wake akitoka na mwanamume mwingine.