Video: Mhitimu wa chuo kikuu achoma vyeti, mwaka mmoja baada ya kuhitimu

Mhitimu kama inavyoonekana kwenye hati alimaliza shule yake ya upili mnamo 2017 na akapata alama ya B kabla ya kuendelea na chuo kikuu na kuhitimu Julai 2022.

Muhtasari

• Wengine walihisi ni mapema mno kwa kijnana huyo kutamauka katika soko la ajira kwani ni miezi 11 tu tangu kuhitimu.

Mhitimu wa chuo kikuu achoma vyeti vyake mwaka mmoja baada ya kuhitimu.
Mhitimu wa chuo kikuu achoma vyeti vyake mwaka mmoja baada ya kuhitimu.
Image: Screengrab

Video inayoonyesha Mwanafunzi anayedhaniwa kuwa wa Chuo Kikuu kimoja nchini Kenya akichoma vyeti vya shule imezua hisia tofauti mtandaoni.

Katika video hiyo mwanafunzi huyo aliteketeza Cheti chake cha Elimu ya Msingi cha Kenya (KCPE), Cheti cha Elimu ya Sekondari cha Kenya (KCSE), na nyaraka zingine ikiwemo cheti chake cha kuhitimi chuo kikuu cha Mt Kenya mwaka jana.

Mhitimu kama inavyoonekana kwenye hati alimaliza shule yake ya upili mnamo 2017 na akapata alama ya B kabla ya kuendelea na chuo kikuu na kuhitimu Julai 2022.

Haijulikani mhitimu huyo aliamua kufanay hivyo kwa nini lakini wengi ambao walipata kutoa maoni yao walikisia kwamab huenda ni kutokana na kutamauka baada ya kukaa nje kwa mwaka mmoja bila kufanikiwa kupata ajira.

Uamuzi huo wa haraka na usio wa kimantiki uliwaacha wengi wakijiuliza ni vipi kizazi cha vijana kinachukua hatua zisizo za lazima kinapokabiliwa na changamoto.

Wengine walihisi ni mapema mno kwa kijnana huyo kutamauka katika soko la ajira kwani ni miezi 11 tu tangu kuhitimu na pengine angejipa muda Zaidi ili kung’oja nyota yake kung’aa.

“Mwaka mmoja tu nje ya shule, na tayari anachoma vyeti vyake? Hana subira vya kutosha. Je, anaweza kumudu kufanya kazi kwa shinikizo?” Mmoja alihoji.

 

 Wengine hata hivyo walidai kuwa mwanafunzi huyo alikuwa anatafuta njia ya kutrend na kuwa gumzo mitandaoni kwa kuchoma kile walikisia kuwa ni vyeti bandia – kwani katika dunia ya sasa, vijana haswa wengi walioko kwenye mtandao wa TikTok hufanya mambo ya ajabu na mengine ya kushangaza ilmradi tu waweze kupata ufuatiliaji mkubwa wa mtandaoni na kutelekza kwa ganda la ndizi kwa kuvuma na umaarufu unaokuja na vitendo hivyo kwa kushangaza.

Lakini iwapo ni vyeti halisi na vya kweli, basi kijana huyo huenda ni pigo la kutopata ajira kama ambavyo alikuwa ameaminishwa na wahadhiri wake enzi za uanafunzi wake.

Ikumbukwe wimbi la kukosekana kwa kazi limesakama mamilioni ya watu kote duniani, makampuni mengi yakihamisha nyingi ya huduma zao kwenye mitandao kwa njia za kidijitali, hivyo kuwakosesha wengi kazi, ikikadiriwa kuwa bado ni athari za janga la Covid-19 ambazo zinaendelea kuathiri mifumo mingi ya kiuchumi kote duniani, na hivyo kufanya hata gharama ya maisha kwa wengi kushindwa kuimudu.

Hii hapa video ya tukio hilo: