Wafuasi 65 wa Pasta Mackenzie washtakiwa kwa kukataa chakula baada ya kuokolewa

Vyanzo vinadai kwamba 65 hao walikuwa wanageuka wajeuri na wenye vita kali dhidi ya chakula, huku wakitaka kuachiliwa huru ili kurudi msituni na kuendelea na ibada ya kufunga ili 'kuona Mungu'.

Muhtasari

• Walifunguliwa mashtaka ya kujaribu kujiua kwa kukataa chakula katika vituo vya uokozi, kinyume na kifungu cha 226 cha katiba.

wafuasi wa Mackenzie wafikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya kugoma kula.
wafuasi wa Mackenzie wafikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya kugoma kula.
Image: Screengrab//YouTube

Wafuasi Zaidi ya 60 wa kanisa la mhubiri tata Paul Mackenzie na ambao walikataa kula chakula hata baada ya kuokolewa kwenye kwenye shamba la Shakahola wamefikiwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya kujaribu kujiua kwa njaa.

Katika video moja ambayo ilipakiwa kwenye mtandao wa YouTube na Nation, makumi hao ambao wanaaminiwa kuwa na ufuasi kindakindaki kwa Mackenzi na kanisa lake la Good News International walifikishwa katika mahakama huku wakishushwa kutoka kwa magari ya polisi.

Wafuasi hao 65 wa Mackenzi walifikishwa katika mahakama ya Shanzu Jumatatu alasiri.

Walifunguliwa mashtaka ya kujaribu kujiua kwa kukataa chakula katika vituo vya uokozi, kinyume na kifungu cha 226 kama ambavyo kinasomeka na kifungo 36 cha kanuni za adhabu.

Kulingana na hati za mashtaka ambazo ziliandaliwa na mkurugenzi wa mashtaka ya umma, wafuasi hao walijaribu kujiua kwa kukataa chakula wakiwa katika vituo vya uokoaji.

Kulingana na jarida la Nation, watu hao walikataa kula chakula katika kituo cha uokoaji cha Sajahanadi Rescue Centre, Kilifi kati ya Juni 6 na Juni 10, huku wakianzisha mgomo dhidi ya kula.

Kulingana na jarida hilo, vyanzo vya ndani vinadai kwamba wafuasi hao wa Mackenzi hadi walifikia hatua ya kugeuka kuwa wajeuri na wenye vita pindi walipotakiwa kula, huku wakitaka kuachiliwa huru ili wakarudi msituni kuendelea na ibada yao ya kufunga ili ‘kumuona Mungu’.