logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rais Ruto aongoza kuzindua soko Naivasha, kutimiza Manifesto

Tungali tunatekeleza Manifesto ya Kenya Kwanza ili kuyabadili maisha ya Wakenya.

image
na TOM KIRIMI

Habari15 June 2023 - 13:43

Muhtasari


  • •Kulingana na Ruto, soko hili linalojulikana kama Naivasha Modern Market likilenga kufanyiwa biashara na zaidi ya wafanyi biashara 1,000.
  • •Baadhi ya ushuru wanaotarajia ni; ushuru wa nyumba 1.5%, ushuru wa petroli 16% pamoja na makato mengine, ambapo wanasema kila kitu kitapandishwa bei nchini.

Rais William Ruto ameongoza katika uzinduzi na ufunguzi wa soko katika mji wa Naivasha Alhamisi 15.

Kulingana na Ruto, soko hili linalojulikana kama Naivasha Modern Market likilenga kufanyiwa biashara na zaidi ya wafanyi biashara 1,000.

“Our bold decision to construct a modern market in Naivasha Town emboldens the Government’s focus to working with Counties in offering small traders spacious, adequate and decent places to run their businesses.” Ambayo katika tafsiri;

Uamuzi wetu mkuu kujenga soko la kisasa katika mji mkuu wa Naivasha unavumbua lengo la serikali kushirikiana na kaunti ili kuwapa wafanyi biashara  wadogo nafasi kubwa tena za kutosha katika mahali pazuri ili kuendeleza biashara zao.

Rais aliendelea na kusema kuwa, hili litaimarisha biashara na kuongeza mapato ya wanabiashara nitakachaochangia kunawiri kwetu.

“Also addressed wananchi in the town where we committed to implement every item of the Kenya Kwanza Manifesto so that we can transform the lives of the people.” Aliendelea. Ambapo inatafsiriwa kuwa; Nilihutubia wananchi waliokuwa mjini kwamba tungali tunatekeleza Manifesto ya Kenya Kwanza ili kuyabadili maisha ya Wakenya.

Ruto aliandanama na baadhi ya magavana wakiwemo; Gavana wa Nakuru Susan Kihika, wa KIambu, Wamatangi, pamoja na wabunge; Karanja wa Nakuru, Jayne Kihara wa Naivasha, John Kiragu , Limur na Methu Muhia wa Nyandaraua.

Haya yanajiri huku Wakenya wakitarajia kutozwa ushuru zaidi wakati bajeti ya taifa itakapomalizwa kupitishwa kuwa sheria katika Bunge. 

Baadhi ya ushuru wanaotarajia ni; ushuru wa nyumba 1.5%, ushuru wa petroli 16% pamoja na makato mengine, ambapo wanasema kila kitu kitapandishwa bei nchini.

Wakati huo huo kutokana ushuru huo, kulingana na wabunge waliopinga mswada wa wa fedha 2023, walikiri kwamba, baadhi ya wanabiashara wakuu nchini wamehama kwenda kutafuta taifa mbadala kufanyia biashara zao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved