Mume amwekea dawa mkewe na kumrekodi akibakwa na wanaume 51 kwa miaka 10

Mume huyo walikuwa wameoana na mkewe kwa zaidi ya miaka 50 na alipata wanaume hao kwenye tovuti mbovu ya wabakaji kabla ya kuwaza kuwapa kibarua cha kumbaka mkewe akiwa amelala.

Muhtasari

• Wanaume 51 - wenye umri wa kati ya miaka 26 na 73 - wameshtakiwa kwa ubakaji na kurudishwa rumande.

• Uchunguzi wa kimatibabu pia ulionyesha alikuwa ameambukizwa magonjwa manne ya zinaa.

• Anafahamika kuwa alipambana na mfadhaiko kufuatia mashambulizi hayo na amewasilisha kesi ya talaka.

Mwanaume aliyekamatwa
Mwanaume aliyekamatwa
Image: Sagwe

Mwanamume mmoja wa Ufaransa ameshtakiwa kwa kumnywesha mke wake dawa za kulevya kila usiku na kisha kuwarekodi wanaume wasiopungua 51 wakimbaka akiwa amelala.

Mshukiwa huyo anayejulikana kwa jina la Dominique P, anadaiwa kutekeleza mashambulizi hayo baada ya kuchanganya dawa ya kutibu wasiwasi kwenye mlo wa mkewe, gazeti la Telegraph liliripoti.

Kisha angewaalika wale walioitwa wageni wake nyumbani kwao Mazan, Ufaransa kufanya vitendo vya ngono kwa mwanamke aliyelala, anayerejelewa chini ya jina bandia la Françoise.

Inaeleweka kuwa Dominique angerekodi mashambulio hayo na kuweka picha kwenye hifadhi ya USB katika faili inayoitwa 'MATUSI'.

Wanaume 51 - wenye umri wa kati ya miaka 26 na 73 - wameshtakiwa kwa ubakaji na kurudishwa rumande. Wachunguzi wamegundua kesi 92 za ubakaji wa Françoise na 'wachokozi' 83 lakini bado hawajabaini wote wanaodaiwa kumshambulia, jarida hilo lilisimulia.

Dominique, ambaye alikuwa ameoana na Françoise kwa zaidi ya miaka 50, inaeleweka kuwa aliwapata wanaume hao kwenye jukwaa mbovu la ubakaji mtandaoni, kulingana na gazeti hilo.

Mashambulio hayo yanayodaiwa yalitokea kati ya 2011 na 2020, huku upande wa mashtaka ukidai kuwa Dominique anasisitiza kwamba hakuna mshambuliaji 'aliyeacha kufanya vitendo vya ngono na mke wake kutokana na hali yake'.

Waendesha mashtaka wa Avignon wanasema Dominique 'hakuwahi kutumia vurugu au vitisho' kuhakikisha ubakaji unafanyika, na kuongeza: 'Kila mtu alikuwa na hiari yake ya kuacha vitendo hivi na kuondoka.'

Baadhi ya wabakaji wanafahamika kufika nyumbani mara nyingi. Wengi wanadai kuwa hawakujua kwamba Françoise hakuwa amekubali kukutana nao kimwili.

Françoise, ambaye alifahamu kuhusu mashambulizi hayo baada ya polisi kupata kanda hizo, alisema alipata matatizo ya uzazi, uchovu wa mara kwa mara na 'kutokuwa na akili'.

Uchunguzi wa kimatibabu pia ulionyesha alikuwa ameambukizwa magonjwa manne ya zinaa.

Anafahamika kuwa alipambana na mfadhaiko kufuatia mashambulizi hayo na amewasilisha kesi ya talaka.