Kalonzo amkosoa vikali Raila kwa kuhimiza matumizi ya vurugu na fujo dhidi ya polisi

Tamko la Kalozo linakuja siku chache tu baada ya Odinga kunaswa akiwapongeza na kuwahimiza waandamanaji kutumia fujo dhidi ya polisi wakati wa maandamano.

Muhtasari

• Kalonzo alisema haya Ijumaa wakati aliongoza maandamano ya amani kaunti ya Machakos.

Kalozno amkosoa Odinga kuwahimiza waandamanaji kutumi vurugu dhidi ya polisi.
Kalozno amkosoa Odinga kuwahimiza waandamanaji kutumi vurugu dhidi ya polisi.
Image: Facebook

Kinara mwenza wa muungano wa Azimio la Umoja Kalonzo Musyoka amekashifu vikali matumizi ya vita na vurugu kwa waandamanaji kupinga uonozi wa Kenya Kwanza unaongozwa na William Ruto.

Tamko la Kalonzo linakuja siku chache tu baada ya kinara wa Azimio Raila Odinga kuwapongeza waandamanaji kwa kutumia vurugu dhidi ya polisi katika maandamano siku ya Ijumaa wiki iliyopita.

“Ambieni watu wetu, mtu asiwe… kama tunaamini katika mabadiliko ambayo tunataka, hatuwezi kushiriki katika vurugu na vita, hatuwezi faidika na chochote kupitia vita, hatuwezi,” Kalonzo alisema katika klipu iliyochezwa na runinga ya NTV.

Kalonzo alisema haya wakati aliongoza maandamano ya Amani huko Kathiani kauti ya Machakosi siku ya Ijumaa ambayo viongozi wanaoegemea upande wake walionekana wameketi kwenye jukwaa ambalo liikuwa na zulia jekundu.

Mwanachama wa Wiper, gavana wa Machakos Wavinya Ndeti ambacho ni chama cha Kalonzo amesisitiza kwamba hayuko katika lengo la kushiriki kwenye maandamano hayo ambayo tena yameitwa na Azimio Jumatano wiki hii.

“Hapa Machakos, tumesema ni kazi, waheshimiwa, hatutaki kelele, mimi hamtasikia siku moja nikisimama, nipige kelele nifanye nini, sina muda kwa hilo,” Gavana Ndeti alisema.

Kando na hayo, Kalonzo pia alimsuta vikali kiranja wa walio wengi kwenye bunge la kitaifa, Silvanus Osoro kwa matamshi yake kwamba walihonga baadhi ya wabunge wa Azimio ili kupitisha mswada tata wa fedha wa mwaka 2023.

“Yaani unasema mlihonga, na hilo linapita tu bila kuadhibitwa. Yaani ni kusema kwamba kama hiyo inafanyika kwenye bunge, ni sawasawa na tumehalalisha mambo ya hongo,” Kalonzo aliteta.

Jumatano wiki hii, Azimio wanatarajiwa kurejelea duru ya pili ya maandamano yao katika awamu ya pili, baada ya kuchukua mapumziko ya muda mwezi Machi ili kupisha muda kwa mazungumzo ya pande zote mbili ambayo hata hivyo walisema kuwa hayakufua dafu na kulaumu uongozi wa Kenya Kwanza ukiongozwa na rais Ruto.