Mwanamume afariki baada ya kudungwa sindano ya kuongeza ukubwa wa uume wake

Kijana huyo mwenye miaka 32 aliona tangazo la mtu huyo aliyejiita daktari mitandaoni akisema kuwa ana uwezo wa kumdunga mtu dawa ya kuongeza uume wake mara dufu.

Muhtasari

• Mtu anayedaiwa kutekeleza utaratibu huo, anayejulikana kama Torben K, hana sifa za matibabu, kulingana na waendesha mashtaka.

• Alitangaza jabs zake kupitia tangazo la mtandaoni, ilidaiwa.

• Inasemekana kuwa mwathiriwa alianza kupata matatizo ya kupumua muda mfupi baada ya kurejea nyumbani kutoka kwa upasuaji.

Mwanaume afariki kwa kudungwa sindano ya kuongeza uume.
Mwanaume afariki kwa kudungwa sindano ya kuongeza uume.
Image: BBC PIDGIN

Mwanaume mmoja raia wa Ujerumani amefariki dunia kufuatia tatizo la kudungwa sindano ili kunenepesha uume wake.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye hakutambuliwa, inasemekana alidungwa mafuta ya silicone kwenye sehemu yake ya siri na mfanyakazi wa upishi aliyejifanya kuwa daktari, Mail Online waliripoti.

Alikufa kwa sepsis miezi saba baadaye, baada ya kupigwa na msururu wa matatizo ya kiafya.

Mtu anayedaiwa kutekeleza utaratibu huo, anayejulikana kama Torben K, hana sifa za matibabu, kulingana na waendesha mashtaka.

Alitangaza jabs zake kupitia tangazo la mtandaoni, ilidaiwa.

Inasemekana kuwa mwathiriwa alianza kupata matatizo ya kupumua muda mfupi baada ya kurejea nyumbani kutoka kwa upasuaji.

Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, alitafuta usaidizi kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Giessen na baadaye alitumia miezi mingi katika uchungu katika wodi ya wagonjwa mahututi.

Waendesha mashtaka wanadai kuwa sindano hizo zilisababisha mwathiriwa kuugua ugonjwa wa sepsis, mwitikio wa ziada wa kinga ya mwili kutokana na maambukizi.

Mwendesha Mashtaka Mkuu Wolf-Tilman Baumert aliambia vyombo vya habari vya ndani: 'Kwa bahati mbaya, mafuta ya silikoni yaliishia kwenye mkondo wa damu wa mtu huyo.

'Hii ilisababisha matatizo makubwa ya kiafya na, hatimaye, kifo chake.'

Aliongeza: "Ukweli kwamba mwanamume huyo aliomba matibabu haina maana kwa maoni yetu. Mshtakiwa alitenda kwa unyama sana.'

Kesi hiyo kwa sasa inaendelea huku hukumu ikitarajiwa mwishoni mwa mwezi huu.