logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mrembo anyolewa kipara kwa kushindwa kulipa bili ya saluni baada ya kusukwa (+video)

Msusi alionekana akitumia wembe kumnyoa mteja huyo huku wateja wengine katika saluni hiyo wakitazama kwa mshtuko.

image
na Radio Jambo

Habari18 July 2023 - 11:52

Muhtasari


•Mteja huyo mwenye umri wa ujana alikuwa ametengenezwa nywele kwenye saluni hiyo lakini hakuweza kulipia huduma hiyo.

•Msichana alionekana kukata tamaa na kuchanganyikiwa sana baada ya zoezi la kunyoa kukamilika na kuachwa na upara kichwa kizima.

Mtengeneza nywele mmoja wa Afrika Kusini hivi majuzi alichukua hatua kali ya kumnyoa mmoja wa wateja wake wa kike ambaye alishindwa kumlipa baada ya kusuka nywele zake.

Ripoti kutoka Afrika Kusini zinaonyesha kuwa mteja huyo asiyetambulishwa mwenye umri wa ujana alikuwa ametengenezwa nywele kwenye saluni hiyo lakini hakuweza kulipia huduma hiyo. Inaripotiwa kuwa msichana huyo alimuagiza msusi huyo kutengeneza nywele zake licha ya kutokuwa na pesa za kulipia huduma hizo.

Katika video iliyovuma, mtengeneza nywele huyo alionekana akitumia wembe kumnyoa mteja huyo huku wateja wengine katika saluni hiyo wakitazama kwa mshtuko.

Kabla ya kuanza kunyoa nywele za mteja huyo, msusi huyo pamoja na wafanyakazi wenzake walisikika wakimpigia kelele msichana huyo na kumuuliza kwa nini alishindwa kulipa. Mmoja wao hata alisikika akimuuliza ikiwa ana mpenzi ambaye angeweza kumsaidi kumaliza deni hilo.

Mtengeneza nywele huyo aliyeonekana kuwa na ghadhabu kubwa alichukua muda wake kuhakikisha kwamba amenyoa nywele zote za msichana huyo bila kuacha hata unywele mmoja. Alisikika akilalamika kwa lugha yake ya kienyeji na kueleza malalamishi yake kwa mteja huyo huku akimkata nywele.

Mwanadada huyo alishika shavu lake tu na kujibu kwa uso wenye huzuni huku mtengeneza nywele akiendelea kukata nywele zake.

“Unaonekana mzuri sana, mrembo sana,” mwanamke mmoja alisikika akimwambia mteja huyo baada ya kunyolewa nywele yote kichwani mwake.

Msichana huyo alionekana kukata tamaa na kuchanganyikiwa sana baada ya zoezi la kunyoa kukamilika na kuachwa na upara kichwa kizima.

Video ya tukio hilo imekuwa ikivuma kwenye mitandao ya kijamii na kuzua hisia mseto kutoka kwa watumiaji wa mtandao. Baadhi ya wanamitandao wameonekana kuunga mkono hatua ya mtengeneza nywele huyo na waliona kuwa ilikuwa sahihi huku wengine wakikosoa kitendo hicho chake.

@stbailey: Kunyoa nywele zake lakini 💔💔 wangeweza kumfanya asafishe mahali na kufanya kazi huko kwa malipo hayo. Hakuna kitu kizuri kuhusu hili, cha kusikitisha sana 😞

@Bigman_Z: Je, wembe ulifaa kweli?

@UncleP_V2 Natumai atafungua kesi bila kujali amekosea hii ni mbaya zaidi wangeweza kumripoti polisi na kuacha sheria ifanye mambo yake. Inachukiza 🚮

@_themediagirl “Kwa nini ukate nywele za mtu? Kwa nini.”


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved