logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mutahi Ngunyi amwandikia Ruto ujumbe mkali baada ya kuondoa ulinzi wa mamake Uhuru

Ngunyi alimwambia kwamba adui si mama Ngina bali ni wananchi waliojawa na ghadahbu.

image
na Davis Ojiambo

Habari19 July 2023 - 05:57

Muhtasari


  • • Ulinzi wa Mama Ngina unadaiwa kuondolewa siku chache tu baada ya Ruto kumzomea vikali mtangulizi wake Uhuru Kenyatta.
  • • Ruto aliashiria kwamba Uhuru ana mkono katika maandamano ya upinzani na kumuonya kwamba atamkomesha.
Ruto atakiwa kuacha kuwaingiza mama zao kwenye mzozo wa siasa.

Mjuzi na mchambuzi wa maswala ya kisiasa Mutahi Ngunyi amemwandikia rais Ruto ujumbe wenye ukakasi mwingi saa chache baada ya ripoti kuibuka kwamba ulinzi wa mama wa kwanza wa taifa, Ngina Kenyatta kudaiwa kuondolewa.

Kupitia ukurasa wa Twitter, Ngunyi alimtaka Ruto kutoruhusu siasa kuenda kinyume na matakwa ya ulinzi wa watu wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini ambao wanaonekana kupinga na kukosoa uongozi wake.

Ngunyi alisema kwamba Ruto ameondoa ulinzi wa Ngina na huenda majangili wakamshambulia lakini pia akamkumbusha kuwa hakuna tofuati kati yake na Uhuru Kenyatta kwani kesho kesho kutwa majangili hao watamwendea mamake, Sarah Ruto.

“Mpendwa Ruto: UMATI hawana akili. Leo WATAMVAMIA Mama Ngina huko Muthaiga. Kesho watamtafuta mama YAKO popote atakapokuwa. Hakuna TOFAUTI kati yako na Uhuru. Ukianzisha TREND hii, HAITASIMAMA. Pambana kama WANAUME na tuwaachie MAMA zetu. Tafadhali,” Mutahi alimtaka Ruto.

Ngunyi alisisitiza akimwambia Ruto kwamba adui si Mama Ngina bali adui ni watu ambao wanasukumwa na ugumu wa maisha na njaa pia, akimtaka kumtafuta Odinga na kufanya mazungumzo naye lakini kuwaacha kina mama kwa viongozi hao mbali na mihemko hii ya kisiasa.

“Kwa Ujumla: Adui SI Mama Ngina. Adui ni WATU. Ni rahisi KUZUNGUMZA na Raila, kuliko KUZUNGUMZA na watu WENYE HASIRA wakiongozwa na watu usiowajua. Usidhani kuwa UNAJUA. Mpendwa Ruto, UNAZINGATIA tatizo HALISI,” Ngunyi alisema.

Ulinzi wa Mama Ngina unadaiwa kuondolewa siku chache tu baada ya Ruto kumzomea vikali mtangulizi wake Uhuru Kenyatta kwa kile aliashirika kwamba yeye ana mkono katika zogo la maandamano ya upinzani.

Upinzani umetangaza kufanya maandamano kwa siku tatu mfululizo kuanzia Jumatano hii asubuhi kote chini kama njia moja ya kumshinikiza Ruto na uongozi wake kushuka chini na kuwasikiliza wananchi kuhusu mzigo mzito wa ushuru ambao umetwikwa mabegani mwao baada ya mswada wa fedha wa 2023 kupitishwa kama sheria mwezi mmoja uliopita.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved