Mwanamume mmoja ameteketza nyumba na kuwachomea ndani wanafamilia wake baada ya kukataliwa kimapenzi na mpwa wake.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Zimbabwe, tukio hilo la kuogofya lililotokea alfajiri ya Julai 29, 2023, moto uliteketeza nyumba moja katika Kijiji cha Mafararikwa, Marange na kusababisha vifo vya wanafamilia wanne na mtoto mmoja kujeruhiwa.
Polisi wa Jamhuri ya Zimbabwe wamethibitisha kuwa tukio hilo lilitokea baada ya mpwa wa mwanamume huyo kukataa ombi lake asilotaka.
Baada ya kukataliwa kimapenzi na mpwa wake, Tonderai Muchimwe aliyethibitishwa kuwa na umri wa miaka 43 aliingia ndani ya nyumba ya mpwa wakekwa hasira na kuinyunyizia petroli kabla ya kuiwasha moto.
Moto huo uligharimu maisha ya Tonderai Muchimwe (43), Ashton Mundoko (12), Quinton Mundoko (7), na Tamari Mundoko (5).
Manusura pekee, Takunda Mundoko (14), alifanikiwa kuepuka moto huo lakini alipata majeraha ya moto mwili mzima, kituo cha runinga ya taifa nchini humo kiliripoti kama ilivyonukuliwa na majarida.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, kisa hicho kilianza wakati Tonderai Muchimwe aliingia kwa nguvu ndani ya chumba alichokuwa mpwa wake, Violet Muchimwe (35) na watoto wake wanne.
Akiwa na kisu, Tonderai alidai kufanya ngono na mpwa wake, na kusababisha mapambano makali. Katika hali ya kukata tamaa ya kutoroka, Violet alitoroka chumbani, akiwaacha watoto wake.
Kwa bahati mbaya, Tonderai aliendelea kunyunyiza petroli katika nyumba nzima kabla ya kuiteketeza.
Moto mkali uliteketeza jengo hilo haraka, na kuwaacha Tonderai, Ashton, Quinton, na Tamari wakiwa wameteketea bila kutambuliwa. Takunda, akionyesha ushujaa wa ajabu, alifanikiwa kutoroka kupitia dirishani lakini aliungua vibaya sana katika harakati hizo