Dorcas Gachagua: Patia serikali miaka 5 tu na mtaona maajabu ya maendeleo

"Ningependa kuzungumzia serikali kwa sababu watu wengi wanafikiri kwamba serikali hii haijafanya lolote na tunazungumzia mwaka mmoja tu.." - Dorcas Gachagua.

Muhtasari

• Dorcas Gachagua alisema serikali ina mpango madhubuti wa kuleta maendeleo na mabadiliko makubwa katika nchi ya Kenya na wanachi.

Mama Dorcas Gachagua awashauri wazazi kuwakubali watoto wao waraibu kama njia mojawapo ya kupona
Mama Dorcas Gachagua awashauri wazazi kuwakubali watoto wao waraibu kama njia mojawapo ya kupona
Image: Facebook

Mama wa pili wa taifa, Dorcas Gachagua amewataka Wakenya wanaosema serikali ya Kenya Kwanza haijafanya kitu kwa mwaka mmoja kuipa serikali kipindi cha miaka 5 ili kuona mabadiliko wanayoyataka.

Akizungumza Wikendi iliyopita katika shule ya wasichana ya Kahuhia huko Murang’a wakati wa kutoa tuzo, Bi Gachagua alitetea serikali ambayo mume wake ni naibu rais akisema kuwa serikali hiyo haijapotoka kutokana na mipnagilio ya ajenda walizouza kwa Wakenya kwa njia ya manifesto kuelekea uchaguzi wa mwaka jana.

Dorcas Gachagua alisema serikali ina mpango madhubuti wa kuleta maendeleo na mabadiliko makubwa katika nchi ya Kenya na wanachi.

"Ningependa kuzungumzia serikali kwa sababu watu wengi wanafikiri kwamba serikali hii haijafanya lolote na tunazungumzia mwaka mmoja tu, ipe miaka mitano na mtaona mabadiliko katika nchi hii," alisema.

Sambamba na hilo, alitambua elimu isiyo rasmi kama sehemu ya kujifunza ambayo itawafanya watu wenye elimu ndogo kudorora katika nyanja ya ajira.

“Serikali inatafuta njia za kuwapa vibali watu hawa ili nao wapate vyeti. Kaka zako ambao wako huko nje ambao huenda hawakupata fursa ya kuwa shuleni na dada zako sasa watapata vyeti na unawakuta kwenye ajira,” Dorcas aliongeza.

Serikali ya Kenya Kwanza inatarajiwa kukamilisha mwaka mmoja ofisini mnamo Septamba 13 na tayari mwaka mmoja umekamilika tangu uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka jana.