logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mama Rachel Ruto amuomboleza binamu aliyemkaribisha Nairobi kwa mara ya kwanza

"Anaacha urithi wa upendo ambao utaendelea kuishi katika mioyo ya wale waliomjua."

image
na Radio Jambo

Habari17 August 2023 - 06:40

Muhtasari


"Alikuwa mwenyeji mwenye neema ambaye aliwafurahisha wageni wake kwa chakula kitamu, chenye lishe na kufariji,”

Rachel Ruto kwenye mazishi

Mama wa taifa Rachel Ruto amemuomboleza binamu yake ambaye alikumbuka kwamba ndiye aliyemkaribisha Nairobi kwa mara ya kwanza miaka kadhaa iliyopita.

Mama Rachel alisema kwamba binamu yake Sally Jepkemboi Mibey alikuwa mtu mzuri ambaye alimpokea Nairobi kwa mikono miwili na kumfanya kuhisi kama yuko nyumbani mbali na nyumbani.

“Sally Jepkemboi Mibey alikuwa zaidi ya binamu kwangu. Alikuwa dada, rafiki na mfano wa kuigwa. Alikuwa na roho ya kung'aa ambayo iligusa maisha ya wengi kwa upendo wake, wema na ukarimu. Alikaribisha kila mtu nyumbani kwake kwa uchangamfu na ukarimu.”

“Sitasahau mara ya kwanza nilipowasili Nairobi na jinsi alivyonikaribisha kwa mikono miwili. Alinifanya nihisi kama mimi ni sehemu ya familia yake. Alikuwa mwenyeji mwenye neema ambaye aliwafurahisha wageni wake kwa chakula kitamu, chenye lishe na kufariji,” mama Rachel alisema.

Mama Rachel alipakia picha ya jinsi hafla ya mwisho ya Sally ilivyokuwa na kusema kwamba siku zote ataishi kukumbuka fadhila zake.

“Alikuwa mama na mfano wa kuigwa kwa wengi. Hekima na imani yake iliwatia moyo wengi, na alinifundisha jinsi ya kuishi kwa neema na ujasiri. Imani yake ilikuwa ni nanga ambayo ilimpa nguvu na amani. Anaacha urithi wa upendo ambao utaendelea kuishi katika mioyo ya wale waliomjua. Mawazo na sala zetu ziko pamoja na familia. Pumzika kwa amani Sally.”


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved