Dereva wa lori amlawiti kijana wa miaka 24 kabla ya kumtupa nje lori likienda kasi

Kijana walikutana na dereva huyo katika carwash alikokuwa akiosha magari ambapo dereva alikuw mteja wa mara kwa mara. Alijitolea kumpa kazi kama turnboy wake kabla ya kumfanyia unyama huo

Muhtasari

• Wakiwa njiani kutoka Tanzania kuja Kenya, dereva huyo alimwekea kisu mwathirika kooni na kumtishia kumuua iwapo angekataa takwa lake.

Kijana alawitiwa na dereva bosi wake
Kijana alawitiwa na dereva bosi wake
Image: BBC NEWS

Kijana wa miaka 24 ana bahati ya kuishi baada ya kutupwa nje ya lori na dereva wake huku likienda kasi.

Hata hivyo, kabla ya kutupwa nje, kijana huyo anadai kulawitiwa na dereva huyo wa matatu ambaye alikuwa amempa kazi kama msaidizi wake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na mtetezi wa haki za kibinadamu na balozi wa kuhubiri dhidi ya visa vya dhuluma za kijinsia na kinyumbani Njeri Migwi, kijana huyo alikuwa amepatiwa kazi kama msaidizi wa dereva huyo na walikuwa wanasafirisha shehena pamoja katika mataifa mbali mbali.

Kijana huyo alikuwa amefungua biashara yake ya kuosha magari katika barabara ya Nairobi kwenda Nakuru ambapo dereva huyo muda mwingi alikuwa ni mteja wake.

Baada ya muda, walijuana na kijana akamueleza dereva kwamba ndoto yake ilikuwa ni kuwa dereva wa maloru ya masafa marefu lakini haikufaulu na ndio maana aliishia kwa kuosha magari.

“Dereva wa lori angepita ili kuosha gari lake, baada ya muda akawa mteja wa kawaida. Alipopoteza 'turnboy' wake, alimpa K fursa ya kuja kumfanyia kazi. K alifunga carwash yake, akaenda kufuata shauku yake,” Njeri Migwi alieleza kwa sehemu.

Waliondoka hadi Mombasa, Tanzania na kurudi. Katika safari ya kurudi Mombasa, dereva alianza kumsogelea, mara moja akamkataa. Mhalifu huyo, alitoa kisu akakiweka kooni, alimbaka na kumpiga teke lori lilipokuwa likitembea. Msamaria mwema Daudi alimpata, kupitia maoni kwenye ukuta huu alitafuta msaada, Migwi kupitia wakfu wake wa Usikimye alisimulia.

Kwa mujibu wa Migwi, kijana huyo aliokotwa na wasamaria wema amabo walimpeleka hospitalini akapewa dawa za kuzuia maambukizi yoyote na mpaka alipokuwa anachapisha taarifa hizo za kuvunja moyo, K alikuwa ameabiri gari kurudi Nairobi.

“K yuko kwenye basi kuelekea Nairobi, na tungependa kumweka kwa mwezi mmoja kwa usaidizi wa kisaikolojia na kuhakikisha anatumia dawa zake. Pia tutamletea simu. Akishamaliza anaweza kurudi akakodi nyumba na kuanza upya maisha yake. Labda kurudi kwa matibabu na ushauri,” Migwi alisema.