logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pupa yawaponza wana Bodaboda; wauziwa juisi wakidhani ni petroli ya magendo

Waliuziwa mkorogo huo Sh100 kwa lita.

image
na Davis Ojiambo

Habari20 August 2023 - 06:46

Muhtasari


  • • Bodaboda hao wawili wamesema kuwa bei ya juu ya mafuta inewasukuma kushawishika kutafuta soko la magendo.
Mwanabodaboda akiuziwa petroli.

Wahudumu wawili wa bodaboda kaunti ya Kaimbu wamepigwa changa la macho baada ya kukimbilia kile kilichodhaniwa kuwa ni petroli ya magendo na kuweka kwenye tenki za pikipiki zao lakini baadae wakaja kugundua ni mkorogo wa juisi.

Kwa mujibu wa gazeti la Taifa Leo, waendesha bodaboda hao walipoteza kiasi cha shilingi elfu 2 baada ya kuuziwa mafuta hayo ambayo yalikuwa yamechanganywa na juisi kiasi na kuwaaminisha kuwa ni petroli safi.

Waathiriwa hao walikutana na watu watatu waliokuwa wamebeba vibuyu viwili vya lita kumi-kumi wote wakiabiri pikipiki moja eneo la Bypass Ruiru katika barabara kuu ya Thika. Hivyo vibuyu vilikuwa vinaonekana kana kwamba vimejazwa pomoni ikawa rahisi kuwaamini,” Jarida la Taifa Leo liliripoti.

Bodaboda hao wawili wamesema kuwa bei ya juu ya mafuta inewasukuma kushawishika kutafuta soko la magendo la mafuta hayo lakini kikawaramba.

Waliuziwa mkorogo huo Sh100 kwa lita.

Bei ya sasa ya petroli ni Sh195 kwa vituo vingi vya mafuta katika eneo hilo.

Baada ya kununua mafuta hayo, wahudumu hao wa bodaboda wanasema kuwa walifumukana upesi kwa sababu waliamini ni biashara ya magendo kwa hivyo ilihitaji shughuli hiyo kufanywa kwa wepesi, Taifa Leo walieleza.

Waathiriwa wameambia Taifa Leo kuwa matapeli hao walivaa masurupwenye yaliyoonyesha walikuwa wanafanya kazi ama katika gereji ama kituo cha kuuzia mafuta ili kuwaghilibu.

Japo imebainika hawajaripoti tukio hili kwenye kituo cha polisi, makumi ya wanabodaboda wanaohudumu kwenye maeneo ya hapo Thika Superhighway katika kaunti za Nairobi na Kiambu, wamewatahadharisha wenzao wawe macho.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved