Pasta ajitupa kutoka ghorofani na kufa baada ya mrembo aliyemsomesha chuo kikuu kumkataa

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 30 alimfundisha mpenzi wake katika chuo kikuu, ambapo alikataa ombi lake la ndoa.

Muhtasari

• Kulingana na utamaduni wa kijiji chao, jamaa huyo alisema alizikwa msituni kwa kufanya “kufuru”.

Crime Scene
Image: HISANI

Mchungaji mmoja wa Kanisa la Kipentekoste nchini Nigeria amejiuwa kwa kujirusha kutoka juu ya ghorofa kisa mgogoro wa kimapenzi.

Kwa mujibu wa jarida la Punch nchini humo, mchungaji huyo mwenye umri wa miaka 30 aliyetambulika kwa jina moja kama Prosper alijitupa kutoka juu ya jengo la Ghorofa mbili na kufariki papo hapo baada ya kuachwa na mpenzi wake, ambaye alikuwa ametumia muda mwingi kumgharamikia.

Jamaa wa marehemu ambaye alizungumza na wanahabari siku ya Jumamosi, alisema mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 30 alimfundisha mpenzi wake katika chuo kikuu, ambapo alikataa ombi lake la ndoa.

Alisema, “Tukio hilo lilitokea mwezi uliopita. Mwanamume huyo (Igboke) alikuwa na umri wa miaka 30 wakati wa kifo chake. Mpenzi wake ambaye alikusudia kumuoa alimkatisha tamaa baada ya kumaliza kumsomesha chuo kikuu.

"Aliruka chini kutoka kwa jengo la ghorofa mbili na kufa. Ninashangaa kwamba mwanamume wa umri huu na mchungaji anaweza kufanya hivi.”

Kulingana na utamaduni wa kijiji chao, jamaa huyo alisema alizikwa msituni kwa kufanya “kufuru”.

"Hatimaye alizikwa Ijumaa kwenye kichaka katika jamii yake," chanzo kiliongeza.

Visa vya wanaume kujitoa uhai baada ya kutendwa unyama na wapenzi wao waliowahudumia kwa hali na mali si vigeni kutembea, na ni muda tu baada ya wanaume kujifuzna kutokana na matukio kama hayo ya awali.