'Acha kumfuata Rais isivyofaa,'Wakili Donald Kipkorir kwa Gachagua

Rais alitoa hotuba yake na kuelezea kujitolea kwake kwa masuala yanayohusu hatua za hali ya hewa.

Muhtasari
  • Wakili huyo alisema kuwa ni wakati mwafaka wa kurejesha kamati ya mwongozo wa kitaifa na masuala ya kisiasa.
LIPA NA UKOME: Wakili Donald Kipokorir
LIPA NA UKOME: Wakili Donald Kipokorir
Image: MAKTABA

Wakili Donald Kipkorir amemtaka naibu rais Rigathi Gachagua kujishughulisha na kuacha kumfuata rais katika kila shughuli hata pale ambapo hatakiwi kuongea.

Ni wazi kuwa, tukio la mkutano wa kilele wa hali ya anga limemwaibisha pakubwa Gachagua.

Naibu Rais Rigathi Gachagua alimfuata rais William Ruto kwenye kongamano la hali ya hewa KICC lakini kwa bahati mbaya hakupewa fursa ya kuzungumza.

Rais alitoa hotuba yake na kuelezea kujitolea kwake kwa masuala yanayohusu hatua za hali ya hewa.

Wakili huyo alisema kuwa ni wakati mwafaka wa kurejesha kamati ya mwongozo wa kitaifa na masuala ya kisiasa.

"Je, kuna jukumu la Naibu Rais wetu Rigathi Gachagua zaidi ya kumfuata Rais hata ikiwa Rais anaenda kuhesabu ng'ombe wake? Angalau tunajua DP wetu ni mtu anayeruka mapema na kukimbia mbio. Je, si wakati wa KAMATI YA MAZUNGUMZO kutoa jukumu halisi la utendaji kwa naibu rais? Tunaweza kurudisha Wizara ya Mwongozo wa Kitaifa na Masuala ya Kisiasa na kuifanya kuwa sehemu ya ofisi ya DP. (Wakenya waliozaliwa baada ya 1991 wanaweza wasijue tulikuwa na Wizara kama hiyo),"Kipkorir aliandika kwenye ukurasa wake rasmi wa Twitter.