logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Peter Salasya awajibu wanaomshabulia kuhusiana na mahojiano yake kuhusu Tabianchi

Salasya amedai kuwa alijaribu kutumia lugha ambayo inaleweka na kila mtu kando na wenzake wanaotumia kingereza tu.

image

Habari06 September 2023 - 12:11

Muhtasari


  • •Salasya alijieleza akisema kuwa, alikuwa amehudhuria kongamano hilo kwa hiari yake, kwani,  yeye si mwanaharakati wa mazingira.
  • •“Ni vigumu kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa sababu ya umaskini na jinsi watu wanvyoishi, na hivyo ndivyo nilivyosema,”
akizungumza nje ya KICC mnamo Septemba 5, 2023.

Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya amewajibu wanaomshambulia mitandaoni kufuatia  mahojiano ya hivi majuzi kuhusu Tabianchi  wakati wa kongamano la tabianchi lililofanyika  Mjini Nairobi.

Katika mahojiano na SPM Buzz, mbunge huyo wa awamu ya kwanza katika bunge la kumi na tatu alisema;

“Mabadiliko ya hali ya hewa ni ya kweli kwa sababu ya ongezeko la joto duniani, yale yatakayo jadiliwa kwenye kongamano hili, ikiwa yatatekelezwa basi ni kwa manufaa ya nchi,”

Mbunge huyo aliongeza kuwa;

“Kama wabunge ambao tumechaguliwa kuwakilisha maeneo bunge, tunapigia upato sana swala la mazingira katika maeneo bunge yetu kwa kuwashauri watu waepuke kutumia kuni ili  kutumia gesi ama jiko za kisasa ambazo hazitatatiza mazingira, tuko na mpango, na vijana wetu wako na mapendekezo ambayo tunadhamiria kuwasilisha bungeni ili wapate ufadhili wa kuyatekeleza,

Baadaye mwanablogu, Pauline`Njoroge alitoa maoni kuhusiana na mahojiano ya Salasya akisema,:

“Najua hauko tayari kwa mazungumzo haya lakini kama nchi tunapaswa kuwacha kuchagua watu kwa sababu ya huruma na kuanza kuchagua watu wanaofaa kwa majukumu, kusema kweli Peter Salasya hafai kuwakilisha Mumias Mashariki,”

Mbunge huyo  sasa amejitokeza kujieleza kwa kina kuhusiana na mahojiano hayo.

Kwenye kanda ya video aliyoachilia mitandaoni julai 6, Salasya alijieleza akisema kuwa, alikuwa amehudhuria kongamano hilo kwa hiari yake, kwani,  yeye si mwanaharakati wa mazingira na kusema kwamba hafahamu mambo ya tabiainchi.

Salasya vilevile alijitetea akisema,

“Ni vigumu kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa sababu ya umaskini na jinsi watu wanvyoishi, na hivyo ndivyo nilivyosema,”

Aidha amedai kuwa alijaribu kutumia lugha ambayo inaleweka na kila mtu kando na wenzake wanaotumia kingereza tu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved