Mzee wa miaka 72 aanguka na kufariki saa chache baada ya kujiandikisha Inua Jamii

Kwa mujibu wa taarifa, mzee huyo alikuwa amepanga foleni ndefu kwa saa kadhaa kuanzia saa kumi na mbili alfajiri na alikuja kusajiliwa majira mchana kabla ya kuanguka chini na kuzirai.

Muhtasari

• Wakongwe hao walikuwa wamejitokeza asubuhi na walipanga foleni kwa muda mrefu kabla ya kusajiliwa.

Crime Scene
Image: HISANI

Mzee mmoja wa umri wa miaka 72 katika eneo la Nyaribari Chache kaunti ya Kisii ameripitiwa kuanguka, kuzirai na baadae kuripotiwa kufariki dunia baada ya kumaliza kupanga foleni ya kusajiliwa katika mpango wa Inua Jamii ambao unashughulikia marupurupu kwa wazee wa Zaidi ya miaka 70.

Mzee huyo alisemekana kuzirai nje ya ukumbi wa jamii katika eneo la Keumbu ambapo mamia ya wazee wa Zaidi ya miaka 72 walikuwa wamepiga foleni ili kusajiliwa.

“Wakaazi wanailaumu serikali kwa mipango mbovu ambapo wazee kadhaa waliojitokeza tangu 6:00 asubuhi walikuwa wamesimama kwenye mlolongo kwa muda mrefu,” Chanzo kimoja cha habari kilisema.

Haya yanajiri ikiwa ni siku chache baada ya naibu rais Rigathi Gachagua kufichua kwamba tayari rais Ruto ametoa agizo la kusajiliwa upya kwa wazee wenye umri wa miaka 70 kwa mpango wa Inua Jamii kwa ajili ya kupokezwa shilingi elfu 2 kila mwezi.

“Rais ametuagiza tuanzishe tena kuandikisha wazee wa miaka 70 kwenda juu waanze kupata marupurupu yao,” Gachagua alisema wakati wa mkutano wa ugatuzi mjini Eldoret wiki chache zilizopita.

Katika hotuba yake, Naibu rais pia aliwaambia watu kwamba watamsajili kinara wa upinzani Raila Odinga katika mpango huo ili kumpokeza elfu 2 za kila mwezi katka njama ya kumsaafisha kutoka kwa siasa.

Na tukiandikisha hao nimemwambia PS huyu mzee wa kitendawili [Raila Odinga] umwandikishe akuwe anachukua elfu yake mbili kila mwezi ndio aende kupumzika,” Gachagua alisema huku watu wakimshangilia.