Kutana na mwanamume aliyejifungia ndani ya nyumba miaka 55 kwa kuogopa wanawake

Majirani walisema kwamba tangu utotoni wameishi kumuona akiwa ndani ya boma lake na pindi anapomuona mwanamke anajaribu kuingia katika boma lake hukimbia ndani ya nyumba na kujifungia.

Muhtasari

• Kisayansi, hali kama hii kwa mujibu wa kniliki ya Cleveland huletwa na hali inayojulikana kwa kimombo kama Gynophobia.

• Hali kama hii inaweza tokana na matukio mbali mbali yakiwemo matukio ya awali utotoni, ama ushawishi wa kitamaduni.

Mzamwita, jamaa aliyejifungia.
Mzamwita, jamaa aliyejifungia.
Image: Screengrab

Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 71 amewashangaza wengi baada ya kukiri katika simulizi lake kwamba hajawahi onana ana kwa ana na mtu yeyote wa jinsi ya kike.

Callixte Mzamwita kutoka Rwanda alisema kwamba alianza kujifungia ndani ya nyumba akiwa na umri wa miaka 16 na tangu hapo mpaka sasa akiwa na umri wa miaka 77, hajawahi kutana na mwanamke yeyote.

Kwa mujibu wa simulizi hilo kama lilivyosimuliwa na Afrimax English, Mzamwita amejifungia ndani ya nyumba kwa miaka 55 sasa.

Alijifungia ndani ya nyumba muda huo wote kwa sababu hakutaka kukutana wala kufanya mazungumzo na mwanamke yeyote.

“Hata leo sababu ambayo ilimfanya kuniruhusu niingie katika nyumba yake ni kwa sababu mko hapa. Lakini kama si yeye asingeniruhusu kuingia kwake,” mwanamke mmoja aliambia Afrimax.

“Sababu ambayo hunifanya nijifungie ndani na kuweka ua wa kuzunguka nyumba yake ni kwa sababu nataka kuhakikisha kwamba hakuna wanawake wanaoweza kunikaribia. Sitaki wanawake karibu na mimi kwa sababu wanaifanya nahisi woga sana,” mzee huyo alisema.

Majirani walisema kwamba tangu utotoni wameishi kumuona akiwa ndani ya boma lake na pindi anapomuona mwanamke anajaribu kuingia katika boma lake hukimbia ndani ya nyumba na kujifungia.

Kisayansi, hali kama hii kwa mujibu wa kniliki ya Cleveland huletwa na hali inayojulikana kwa kimombo kama Gynophobia.

Hali kama hii inaweza tokana na matukio mbali mbali yakiwemo matukio ya awali utotoni, ama ushawishi wa kitamaduni.

Majirani wa kike walisema kuwa wengi ndio wamekuwa wakimpa msaada japo huwa hapendi mwanamke kumkaribia.

 Walisema kuwa mara nyingi humrushia vifurushi vya vyakula kwenda ndani ya boma lake pasi na kumkaribia kwani kila wanapojaribu kumkaribia hutoroka na kuingia ndani.

“Huwa tunarusha vyakula kupitia juu ya ua la boma lake, huwa hataki tumkaribia lakini huwa anachukua kile ambacho tunamrushia kutoka mbali,” mmoja alisema.

Cha ajabu ni kwamba mwanamume huyo hufanya kila kitu mtu wa kawaida anaweza fanya ndani ya nyumba yake ikiwemo bafu, choo, meko na hata malazi.