Quickmart yaadhimisha miaka 17 kwa kampeni ya “Okoa Shilingi na Quickmart”

Quickmart imekuwa mshirika thabiti kwa jamii kote nchini Kenya kwa miaka 17, na kampeni ya "Okoa Shilingi na Quickmart" ni ushahidi wa dhamira hii ya kudumu.

Muhtasari
  • Quickmart itawazawadia wateja wao kwa matoleo ya kila siku yaliyopunguzwa bei kwenye bidhaa mahususi kila siku.
  • Wateja waliobahatika kufika kwenye till ya kulipia majira ya saa 17:59 katika matawi yake 59 wana nafasi ya kupewa zawadi za kipekee.

Quickmart, ni moja kati ya maduka makuu ya rejareja yanayoongoza nchini wanajivunia kutangaza sherehe yao ya miaka 17 kwa uzinduzi wa kampeni ya kusisimua ya "Okoa Shilingi na Quickmart".

Kampeni hii ya furaha inaadhimisha safari ya Quickmart kama chapa inayoaminika, inayohudumia mamilioni ya Wakenya, na inawapa wateja ofa maalum za kila siku zisizo na kifani.

Zaidi ya hayo, kama ishara ya shukrani, Quickmart itawazawadia wateja wao kwa matoleo ya kila siku yaliyopunguzwa bei kwenye bidhaa mahususi kila siku. Pia, wateja waliobahatika kufika kwenye till ya kulipia majira ya saa 17:59 katika matawi yake 59 wana nafasi ya kupewa zawadi za kipekee.

Quickmart imekuwa mshirika thabiti kwa jamii kote nchini Kenya kwa miaka 17, na kampeni ya "Okoa Shilingi na Quickmart" ni ushahidi wa dhamira hii ya kudumu. Kuanzia tarehe 1 Septemba 2023, katika mwezi mzima wa Septemba, wateja wanaweza kupata thamani ya kipekee kupitia matoleo maalum ya kila siku kwenye mkusanyiko pana wa bidhaa bora. Kampeni hii inalenga kuwawezesha wateja kufanya maamuzi ya busara huku wakifurahia kuokoa pesa kwa ununuzi wao.

"Tunafuraha kuadhimisha miaka 17 ya kuwahudumia wateja wetu kwa ofa maalum za kila siku zisizo na kifani," alisema Betty Wamaitha, Mkuu wa Masoko wa Quickmart. "Kampeni hii sio tu kuhusu punguzo la bei za bidhaa; ni kuhusu kusherehekea safari yetu, kuonyesha shukrani kwa wateja wetu, na kufanya ununuzi bora kuwa nafuu."

Kama mshangao zaidi, Quickmart itasherehekea umuhimu wa kampeni kwa kuwazawadia wateja watakaojipata kwenye till ya malipo mwendo wa saa 17:59 katika matawi yake 59 kwa zawadi maalum. Mpango huu wa kipekee ni ushahidi wa kujitolea kwa Quickmart kwa kufurahisha wateja.

"Okoa Shilingi na Quickmart" inaangazia jinsi Quickmart imekuwa ikikita mizizi katika kujihusisha na masuala mbali mbali katika jamii. Kampeni hii huleta pamoja washirika, wasambazaji, wafanyakazi, na wateja kusherehekea hadithi ya mafanikio ya miaka 17 ya chapa ya Quickmart.

Quickmart inakubali jukumu muhimu lililotekelezwa na wateja na washirika wake katika safari yake na inatafuta kurudisha mkono wa shukrani kwa jamii ambazo zimeunga mkono ukuaji wake.

Wateja wanahimizwa kutembelea tawi lolote kati ya matawi 59 ya Quickmart.