Tenki la lita milioni 2.3 za divai lapasuka na kusababisha mafuriko barabarani - video

Mji huo unaosheheni watu elfu mbili ulishuhudia tafrija ya bure baada ya malori mawili yaliyokuwa yamebeba tenki za divai kuanguka na kusababisha mifereji ya divai kwenye barabara.

Muhtasari

• Idara ya Zimamoto ya Anadia ilizuia mafuriko na kuyaelekeza mbali na mto, ambapo yalikimbilia katika uwanja wa karibu, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

• Wazima moto walisema chumba cha chini cha ardhi katika nyumba karibu na kiwanda hicho kilikuwa kimejaa mvinyo.

Divai inayomwagika
Divai inayomwagika
Image: Screengrab

Wakaazi katika mji ulioko kwenye ufukwe wa bahari nchini Ureno walibaki katika hali ya mshangao baada ya tenki lililokuwa limebeba divai nyekundu ya lita milioni  2.27 kumwagika katika barabara za mitaa ya mji huo na kuzua mafuriko ya divai.

Kwa mujibu wa jarida la New York Post, malori mawili yalikuwa yamebeba matenki yenye yalikuwa yamejaa divai ya kiasi hicho cha lita wakati yalianguka.

Video iliyotumwa mtandaoni ilionyesha kioevu hicho chekundu kikiteremka kwenye mlima mwinuko katika mji mdogo wa São Lourenço do Bairro, nyumbani kwa wakazi 2,000.

Umwagikaji - ambao ulikuwa mkubwa sana hivi kwamba divai iliyotiririka ingeweza kujaza bwawa la kuogelea la ukubwa wa Olimpiki - ilisababisha tahadhari ya mazingira.

Viongozi walichukua hatua kujaribu kuzuia mvinyo, kabla haujaweza kugeuza Mto Certima kuwa divai.

Idara ya Zimamoto ya Anadia ilizuia mafuriko na kuyaelekeza mbali na mto, ambapo yalikimbilia katika uwanja wa karibu, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Wazima moto walisema chumba cha chini cha ardhi katika nyumba karibu na kiwanda hicho kilikuwa kimejaa mvinyo.

Kwa mujibu wa jarida hilo, Tangu wakati huo kampuni ya Levira Distillery imeomba radhi kwa tukio hilo na kusema ilikomboa ardhi iliyojaa mvinyo.

"Tunachukua jukumu kamili la gharama zinazohusiana na kusafisha na kutengeneza uharibifu, na timu kufanya hivyo mara moja," ilisema katika taarifa.

"Tumejitolea kusuluhisha hali hii haraka iwezekanavyo."

Imeongeza kuwa udongo uliolowa mvinyo shambani umepelekwa kwenye kiwanda maalum cha matibabu.